Agizo
hilo lilitolewa jana na Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba
ambaye alisema kuwa, wote waliotajwa kuhusika katika kulisababishia
taifa hasara kupitia sekta ya madini, hawaruhusiwi kutoka nje ya mipaka
ya Tanzania isipokuwa kwa kibali maalum kutoka serikalini.
“Naelekeza
wote waliotajwa kuhusika hakuna kutoka nje ya mipaka ya nchi yetu
isipokuwa kwa kibali maalum kutoka serikalini. Vyombo vitekeleze maagizo
ya Rais kwa utimamu,” aliandika Waziri Nchemba kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii.
Agizo
hili limekuja ikiwa ni saa chache tangu Rais Magufuli alipoagiza kuwa,
viongozi wote na watumishi mbalimbali waliohusika katika kusaini
mikataba mibovu na kushiriki kwa namna yoyote ile, wahojiwe.
Miongoni
mwa watakaoathiriwa na zuio hilo, ni pamoja na Maafisa wa TRA,
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Andrew Chenge, Mwanyika, na Werema,
Mkurugenzi Idara ya Mikataba, Mary Ndosi, Kamishna Dalali Peter Kafumu,
Waziri Prof. Muhongo, Waziri Daniel Yona, Waziri Nazir Karamagi, Jaji
Julius Malaba, Waziri William Ngeleja.
Awali
Waziri Nchemba alimpongeza Rais Magufuli kwa jitihada alizozichukua
katika kuhakikisha analinda rasilimali za wanyonge na kusema kuwa hakuna
uzalendo kama huo.
“Hakuna
uzalendo zaidi ya kulinda rasilimali za Taifa, Hakuna utetezi wa
wanyonge zaidi ya kulinda rasilimali zao.Hongera sana Mh.Rais kwa
uzalendo wa vitendo kwa Taifa letu.”
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni