Powered by: Elbahsan Web & Blog Designer
Do want your Network!!! Website or Blog-Spot, Try Us: Elbahsan Web & Blog Designer Contact Us Now... Calll; +255743550360 | +255788680558 Email; murtadhaalbahsan@gmail.com

Zawamba Photo Production

Jumatano, 1 Agosti 2018

RSA TANZANIA YAKUTANA KWA MAZUNGUMZO NA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Mhe. Kangi Lugola Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi akikabidhiwa T-Shirt ya mabalozi wa Usalama Barabarni na viongozi wa RSA Tanzania

Leo tarehe 1 Agosti 2018, Uongozi wa RSA Tanzania ukiongozwa na Mwenyekiti wake John Seka na Wakurugenzi Abdulkarim Shah, Ally Nurdin, Marlin Komba, Augustus Fungo pamoja na Isabela Nchimbi mjumbe kutoka TAWLA, akiwakilisha Asasi nyingine zinazojishughulisha na mpango wa marekebisho ya sheria ya Usalama Barabarani, umeonana na Mhe. Kangi Lugola Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi ofisini kwake Jijini Dar es Salaam.

Katika mazungumzo hayo, viongozi wa RSA waliitambulisha RSA Tanzania na Muungano wa Asasi za kiraia zinazoshughulikia usalama barabarani. Pia walimpongeza Mhe. Lugoka kwa kuteuliwa kushika wadhifa huo na hatua mbalimbali anazochukua kuhakikisha usalama barabarani unaimarika.

Aidha, viongozi walimweleza mheshimiwa Waziri changamoto mbalimbali zinazokabili usalama barabarani, na zile zinazokwamisha ufanisi wa taasisi na kutoa mapendekezo ya namna zinavyotakiwa kukabiliwa kiutendaji na kupitia mabadiliko ya sheria ya usalama barabarani.
Viongozi walimkaribisha mhe. Waziri katika RSA na katika Maadhimisho ya Siku ya Mabalozi wa Usalama Barabarani yatakayoadhimishwa 11.08.2018 jijini Dodoma.

Kwa kumkaribisha RSA Tanzania viongozi walimkabidhi Mhe. Waziri, sare ya RSA Tanzania.
Mhe. Waziri aliwashukuru mabalozi kwa kazi nzuri wanayoifanya, akawakaribisha kufabya kazi naye na kuendelea kuunga mkono juhudi za serikali katika kukabiliana na ajali. Akaongeza kuwa atatoa ushirikiano wa kutosha kwa taasisi kwa kuhakikisha pamoja barabarani kunakuwa salama.

Baada ya hapo viongozi walipiga picha ya pamoja na kuagana na mhe. Waziri.
RSA Tanzania
Usalama Barabarani ni Jukumu Letu Sote

Picha na Ally Nusrdin (Ally Six)








Hakuna maoni:

Chapisha Maoni