Powered by: Elbahsan Web & Blog Designer
Jumamosi, 6 Oktoba 2018
Askari JWTZ ajitosa baharini na Kufariki Dunia
Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), amefariki dunia baada ya kujirusha baharini akisafiri na boti ya Azam.
Kifo
cha askari huyo ni moja ya matukio matatu ya watu waliojitupa baharini
wakiwa safarini kwa kutumia usafiri huo, akiwamo mtoto aliyeokolewa
akiwa hai.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya Azam Marine, Abubakar Aziz, alisema jana kuwa
askari huyo alifariki dunia hivi karibuni na kwamba hayo ni miongoni mwa
matukio ambayo yamewahi kujitokeza katika boti zao.
Aziz
alisema katika matukio hayo, watu wawili akiwemo mwanajeshi huyo
walijitosa baharini wakati meli ikiendelea na safari na askari huyo
alijitosa eneo lenye kina kirefu kiasi kwamba asingeweza kuokolewa.
"Matukio
haya yalitokea kwa nyakati tofauti ambapo baada ya kujitupa baharini
licha ya juhudi kufanyika za kuwatafuta, hatukuwapata. Walipatikana siku
nne baadaye akiwa tayari wameshafariki dunia," alisema.
Credit: Nipashe
Credit: Nipashe
Diamond aachia siri aliyoificha muda mrefu mbele ya mamia ya Watanzania
Wakati Diamond anataka kutaja siri iliyomfikisha katika kilele cha mafaniko mamia ya wananchi wa Tandale, viongozi wa ngazi wa Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na wageni waalikwa walikuwa kimya.
Diamond alianza kueleza hatua kwa hatua sababu ambazo zimemfanya awe na mafanikio katika maisha yake ni siri kubwa ya kufanikiwa kwake anasema hachagui kazi ya kufanya.
"Katika maisha yangu sijawahi kuchagua kazi ya kufanya. Ndio maana kwenye maisha yangu nimefanya kazi nyingi sana.Nimefanya kazi ya kuuza mafuta sheli.nimefanya kazi ya kupiga picha kwenye kumbi za harusi pamoja na nimefanya kazi ya kuuza nguo Tandale.
"Siri nyingine ni kujenga uaminifu kwa watu ambao unafanya nao kazi. Uaminifu umenisaidia sana na ndio maana leo niko hapa,"amesema Diamond.
Amesema siri nyingine ni ubunifu na kufafanua baada ya kufanya kazi kwa bidii aliamua kuwa mbunifu kwa kila alichokuwa akikifanya.
Pia amesema kuomba Mungu ni jambo la msingi sana na katika maisha yake moja ya jambo ambalo lazima alifanye ni kumuomba Mungu na amemsadia kumfikisha hapo alipofika.
"Nimekuwa nikimuomba Mungu anisaidie katika shughuli zangu za muziki .Napoomba nataja kaabisa kile ambacho nahitaji ili kumrahisisha Mungu kile ambacho nahitaji kwake.Sitaki kumchanga kwa kuomba mambo mengi.
"Leo hii nimefanikiwa kwasababu namshikirisha Mungu,"amesema Diamond na kuongeza kuwa kwa anayetaka kufanikiwa lazima ajiepushe na matumizi ya dawa za kulevya.
Mh. Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam amabye pia ni mlezi wa kundi la wasanii wa kundi la WASAFI akizungumza na watanzania katika hafla hiyo |
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)