Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), amefariki dunia baada ya kujirusha baharini akisafiri na boti ya Azam.
Kifo
cha askari huyo ni moja ya matukio matatu ya watu waliojitupa baharini
wakiwa safarini kwa kutumia usafiri huo, akiwamo mtoto aliyeokolewa
akiwa hai.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya Azam Marine, Abubakar Aziz, alisema jana kuwa
askari huyo alifariki dunia hivi karibuni na kwamba hayo ni miongoni mwa
matukio ambayo yamewahi kujitokeza katika boti zao.
Aziz
alisema katika matukio hayo, watu wawili akiwemo mwanajeshi huyo
walijitosa baharini wakati meli ikiendelea na safari na askari huyo
alijitosa eneo lenye kina kirefu kiasi kwamba asingeweza kuokolewa.
"Matukio
haya yalitokea kwa nyakati tofauti ambapo baada ya kujitupa baharini
licha ya juhudi kufanyika za kuwatafuta, hatukuwapata. Walipatikana siku
nne baadaye akiwa tayari wameshafariki dunia," alisema.
Credit: Nipashe
Credit: Nipashe
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni