Skauti wakiwa katika chumba cha habari cha magazeti ya The Guardian |
Na Rehema Ramadhani
Dar es salaam; Chama cha Skauti Tanzania
kiliambatana na Skauti kutoka Poland,
Kenya na Burundi ambao ni washirki wa mafunzo maalum ya Public Relation, mapema jana 1/12/2016 walifanya ziara na kujione kazi mbalimbali zinazofanywa
na kampuni ya IPP Media iliyopo Mikocheni Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
na wanachama wa Skauti Tanzania, Msemaji wa Chumba cha Habari Magazeti ya The Guardian na
Nipashe Bw. Faustin Felisian amesema wamefarijika na ujio huo wa wanachama
kutoka Skauti kwa kuja kujifunza na kuona jinsi gani habari zinavyoandaliwa
mpaka gazeti linapotoka mitaani.
“Tumefarijika
sana kwaujio wenu katika chumba chetu cha Habari kwani ni jambo jema kujifunza na
natumai wapo amabo watavutiwa na vinavyofanyika na wengine watatamani kuwa wana
habari hapo baadae” alisema Bw. Felisian.
Mmoja
wa wanachama wa Chama cha Skauti Tanzania Ndg.
Murtadhwa Rashid amesema kuwa ziara hiyo katika chombo cha habari imekuwa
ya mafanikio na faida kwao kwani wamepata fursa ya kujionea mambo mbalimblai
yahusuyo uandishi wa habari.
“Tumefurahi
kwa kupata elimu na tumepokelewa vizuri
IPP Media. Tuna mipango ya kuifikisha Skauti yetu mbali kwa malengo ya
vijana wa Taifa letu na tunawakaribisha watu wote waje kwenye uskauti tujifunze
kwa pamoja” Alisema Ndg. Murtadhwa
Rashid .
Picha na Nelson Opany na Ausi Hussein
This Blog Powerd by:
Elbahsan Web & Blog Designer
A Subsidiary of Elbahsan Web & Blog Designer for Global Development, Inc.
+255 (0) 653 373 432 & +255 (0) 778 246 889
For the Web & Blog Template and Designing
Dar Es Salaam, Tanzania
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni