Na Rehema Ramadhani
Dar es salaam; Chama cha Skauti Tanzania kwa kushirikiana na
chama cha Skauti Poland kimepata mafunzo maalum ya Mawasiliano na Teknolojia ya
Habari maarufu kama PR-Lab kwa baadhi ya wanachama, mafunzo hayo
yalichukua takribani siku sita yalianza 27/11 hadi 2/12/2016 katika viwanja vya
Jakaya Mrisho Kikwete Youth Park kilichopo Mnazi Mmoja jiji Dar es salaam.
Akizungumza na
wanachama wa Chama cha Skauti Tanzania, Mratibu wa mafunzo hayo Bi.Victoria Drodz
kutoka Chama cha Skauti cha Poland, amesema wanafarijika kutoa elimu
hiyo kwa maskauti wa Tanzania kwani Skauti ni ndugu na tunapaswa kupeana yaliyo mazuri ili kujenga Skauti kwa pamoja.
“sisi Skauti
kutoka Poland tunajiskia vizuri kuungana na kutoa elimu hii ya Mawasiliano na
Teknolojia ya Habari. kwa Skauti wenzetu
wa Tanzania kwani Skauti hubadilishana mafunzo na ujuzi wa aina mbalimbali kwa ajili ya kuijenga dunia zaidi ya
tulivyoikuta” Alisema Bi.Victoria.
Tumezungumza na
baadhi ya wanachama wa Chama cha Skauti Tanzania walio hudhuria mafunzo hayo na jinsi walivyo yapokea.
‘Tumefurahi sana
kwa elimu tulioipata kutoka kwa Skauti wenzetu wa Poland kwani elimu hii hutolewa Vyuo Vikuu au
kwa kulipia ili kupata elimu hii, lakini skauti wenzetu kutoka Poland wametupa elimu hii bure kwa ajili ya kuijenga Skauti na Dunia kwa
ujumla” Alisema mmoja wa wanachama wa Chama cha Skauti Tanzania.
Tuli zungumza na Mgeni
Rasmi aliyekuja kufunga mafunzo hayo Balozi Mstaafu Nicholas Kuhanga ambaye pia
ni Mwenyekiti wa Kamati ya Utendani ya Chama cha Skauti Tanzania alisema, amefarijika kuona vijana wake wakipewa elimu yenye
viwango vya juu na anaamini kupitia vijana hao wachache waliopata elimu hiyo
wataisambaza zaidi kwa Skauti wenzao na kwa vijana wote kwa ujumla.
Balozi Mstaafu na
Mwenyekiti wa Kamati ya Utendaji ya Chama cha Skauti Tanzania ndugu Nicholas
Kuhanga akizungumza kabla ya kukabidhi vyeti kwa wahitimu wa Mafunzo ya
Mawasiliano na Teknolojia ya Habari yaliyoandaliwa kwa ushirikiano wa Chama cha
Skauti cha Poland na Tanzania. Mafunzo hayo yalifanyika katika ukumbi wa Kituo
cha Michezo cha Jakaya Kikwete kilichopo Mnazi Mmoja D’salaam.
Picha Na Mutadhwa Elbahsan
This Blog Powerd by:
Elbahsan Web & Blog Designer
A Subsidiary of Elbahsan Web & Blog Designer for Global Development, Inc.
+255 (0) 653 373 432 & +255 (0) 778 246 889
For the Web & Blog Template and Designing
Dar Es Salaam, Tanzania
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni