Chama cha Skauti Tanzania, kimezindua programu mpya iitwayo “U-Report”, mradi huu ni miongoni mwa miradi inayofadhiliwa na UNICEF ambapo upo katika nchi nyingi za Bara la Afrika ata Ulaya.
Chama cha Skauti Tanzania, kimezindua programu mpya iitwayo “U-Report”, mradi huu ni
miongoni mwa miradi inayofadhiliwa na UNICEF ambapo upo katika nchi
nyingi za Bara la Afrika ata Ulaya, mradi wa “U-Report” umezinduliwa
wakati wa maadhimisho ya wiki ya kumbukumbu ya mwanzilishi wa skauti
duniani “Founders day” katika viwanja vya Makao Makuu ya Skauti
Tanzania, Upanga, Dar es Salaam, tarehe 25 Februari 2017.
U-Report ni programu maalum kwaajili ya
kuripoti matukio mbali mbali yanayotokea kwenye jamii zetu kama vile
unyanyasaji wa watoto/kijinsia, matukio ya uhalifu, ajira za utotoni,
ukatili dhidi ya watoto.
Aidha, imetolewa rai ya kujiunga kwa
kutuma sms yenye neno “Sajili” kwenda namba “15070” sms zote ni Bure
(bila ya kutozwa gharama yoyote), huduma hii inapatikana kwa watumiaji
wa mitandao ya simu ya kiganjani ya Tigo, Vodacom, Airtel, Zantel aidha
mradi huo unatarajia kujiunga na mitandao mingine ya simu ya kiganjani
ya Halotel pamoja na TTCL.
Katika uzinduzi huo ulioambatana na
kuazimisha wiki ya kumkumbuka mwanzilishi wa Skauti duniani Robert
Baden-Powell (a.k.a BP) aliyezaliwa tarehe 22 Februari 1857. Ambapo kwa
Tanzania Bara uliingia mwaka 1917, takribani Skauti zaidi ya 5000
waliudhuria kutoka Mkoa wa Dar es Salaam na baadhi kutoka mkoa wa Pwani.
Habari na Murtadhwa El bahsan
Picha na PR Lab (TSA)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni