Na,Vero Ignatus, Arusha.
Watuhumiwa hao 61
wa makosa ya Ugaidi Arusha mapema leo asubuhi walimuhakikishia Hakimu
Nestory Banda kuwa tarehe 11/04/2017, Hawatahudhuria tena mahakamani
hapo hadi upeleezi utakapokamilika.
" Ni zaidi ya miaka minne sasa kila tukija mahakamani hapa mnatuambiwa
kuwa upelelezi haujakamilika ,hata R.C.O alivyokuja kutuona mwezi wa
kwanza mwaka huu alituahidi kuwa ndani ya miezi miwili upelelezi utakuwa
umekamilika sasa tunashangaa mpaka sasa hivi hakuna lolote
linaloendelea"
Hakimu anaendesha kesi hiyo Nestory Banda amewaambia watuhumiwa hao siku ya tarehe 11 ni lazima wahudhuria mahakamani .
"Nawaaahidi
kwamba mara baada ya kumaliza shughuli za ki-Mahakama kwa leo
nitampigia simu R.C.O wala msiwe na tabu nyie njooni mahakamani "
Pichani ni baadhi ya watuhumiwa walivyowasili Mahakamani.
Gari iliyobeba mahabusu wa kesi ya ugaidi likiondoka Mahakamani kuelekea gereza kuu la Arusha
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni