Powered by: Elbahsan Web & Blog Designer
Do want your Network!!! Website or Blog-Spot, Try Us: Elbahsan Web & Blog Designer Contact Us Now... Calll; +255743550360 | +255788680558 Email; murtadhaalbahsan@gmail.com

Zawamba Photo Production

Jumanne, 28 Machi 2017

Mwanamuziki Ney wa Mitego aachiliwa huru


Ney baada ya kuachiliwa baada ya kukamatwa na jeshi la polisi kutokana na wimbo wake mpya wa "Wapo"

Na. Murtadhwa Elbahsan, Dar es salaam.


Mwanamuziki Emmanuel Elibariki maarufu kama Ney wa Mitego, ambaye alikuwa amekamatwa na kuzuiliwa na maafisa wa polisi Tanzania kuhusiana na wimbo wake, ameachiliwa huru.

Wa Mitego aliachiliwa huru saa chache baada ya Waziri wa Habari nchini Tanzania Dkt Harrison Mwakyembe kuagiza aachiliwe huru mapema jana 27 March 2017.

"Saa hizi sina kubwa la kuongea. Wimbo umeruhusiwa. Nashukuru. Nafurahi kusikia taarifa ya serikali kwamba wameruhusu wimbo wa Wapo upigwe. Upigwe kwa nguvu," amesema Wa Mitego baada ya kuachiliwa huru.
Kuhusu kuuboresha wimbo huo, amesema: "Hili nitalifanyia kazi. Siwezi kusema saa hizi ni vitu gani kwa sababu ndio nimetoka huko. Lakini nitalifanyia kazi kwa sababu tayari ni wimbo wa kila mtu, wimbo wa Watanzania, wimbo wa watu wote."

Dkt Mwakyembe hata hivyo alimtaka Ney wa Mitego auboreshe zaidi wimbo wake, kwa mujibu wa ujumbe uliopakiwa katika ukurasa Rasmi wa Msemaji Mkuu wa Serikali ya Tanzania kwenye Twitter.
Sehemu ya maudhui ya wimbo huo inagusia tuhuma za kughushi vyeti ambazo zimekuwa zikigonga vichwa vya habari nchini Tanzania
Wimbo huo mpya wa Ney wa Mitego, ulianza kusambaa katika mitandao ya kijamii wiki iliyopita.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Ulrich Matei alikuwa amesema mwanamuziki huyo alikamatwa kwa kosa la kutoa wimbo wenye maneno ya kashfa dhidi ya serikali.



 





















Hakuna maoni:

Chapisha Maoni