Askofu
wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amekaribishwa kuwa
anaweza kuendesha huduma ya usafiri wa treni na kutaka wadau wengine
wenye nia kama hiyo wajitokeze.
Katika
ibada iliyofanyika juzi, Askofu Gwajima aliwaambia waumini wake kuwa
amedhamiria kununua treni ya umeme itakayogharimu Sh11 bilioni, baada ya
Rais John Magufuli kuzindua mradi wa ujenzi wa reli pana (standard
gauge) itakayokuwa na kasi zaidi ya treni ya sasa na uwezo wa kuchukua
shehena kubwa.
Ujenzi
wa reli uliozinduliwa na Rais Magufuli Aprili 12, utakamilika ndani ya
miezi 30 na awamu ya kwanza itaanzia Dar es Salaam hadi Morogoro, treni
yake itakuwa na kasi ya kilomita 160 kwa saa, ikibeba mabehewa 100.
Msemaji
wa Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli (Rahco), Catherine Moshi
alisema kampuni hiyo imebariki uamuzi huo wa kuwekeza katika usafiri wa
reli, lakini askofu huyo anatakiwa kuomba kibali Wizara ya Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano.
“Tunamkaribisha
mchungaji, hii ni biashara kwetu na huyu ni mwekezaji tena wa ndani.
Hatuwezi kumuangusha cha muhimu ni kufuata utaratibu tu,’’ alisema Catherine.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni