Usiku
wa kuamkia Leo Mbunge wa Jimbo la Mtama mkoani Lindi kupitia tiketi ya
CCM Nape Moses Nnauye ametumia ukurasa wake wa twitter kuandika ujumbe
wake wa wazi aliyowahi kuandika kipindi cha nyuma kuhusu CCM, lengo
likiwa ni kuweka kumbukumbu sawa kwa watu kuhusu CCM.
“Watu
wengi wanaamini nimeisaidia sana CCM lakini ukweli ni kuwa CCM
imenisaidia sana mimi kuliko mimi nilivyoisaidia, CCM ni SHULE.
“Bahati
niliyopata kwa kuwa muenezi CCM ni kufanya kazi na ndg Kinana ni mwema,
mzalendo, hodari, uwezo mkubwa, upendo na maarifa mengi”
Ameandika Nape kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni