Powered by: Elbahsan Web & Blog Designer
Do want your Network!!! Website or Blog-Spot, Try Us: Elbahsan Web & Blog Designer Contact Us Now... Calll; +255743550360 | +255788680558 Email; murtadhaalbahsan@gmail.com

Zawamba Photo Production

Jumanne, 25 Aprili 2017

NAY WA MITEGO AOMBA RADHI KWA MZAZI MWENZIWE

 
Baada ya kuporomoshewa maneno ya kashfa kwenye mitandao na mzazi mwenzake kwa kushindwa kumtunza mtoto zaidi ya kumuweka tuu kwenye mitandao ya kijamii na kujisifu, Nay wa mitego amekiri kubadilika na kuanza kumuhudumia binti yake.

Nay wa Miteho leo Rapa kupitia ukurasa wake wa Instagram ameamua kuudhihirishia umma kuwa kuanzia sasa atakuwa baba mwema na ataanza kuwahudumia watoto wote kwani yeye ni kama kioo hivyo hana budi kutekeleza hayo. 

Nay wa Mitego wiki iliyopita aliandamwa na matusi huku akitolewa maneno ya kashfa na mzazi mwenzake ambaye ni muigizaji wa filamu bongo, Skyner Ally akimtaka kuwa asishoboke kum-'post' mtoto wao aitwae Munnie kwani yeye hana mchango wowote ule kwa mtoto huyo tena alienda mbali zaidi kwa kusema hajui hata gharama za nguo za ndani za mtoto huyo. 
“Si kwa kichambo kile jamaniiiiii huu...Jamani inatosha basi povu. Nitapeleka matumizi. Nawapenda sana awa watoto wanguu. Wasiopeleka matumizi ya watoto wapo “

-ameandika rapa Nay wa Mitego.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni