Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akizungumza Watumishi Halmashauri sekretarieti ,wakuu wa Idara mbalimbali za Serikali ya mkoa Pamoja na viongozi Wa Dini katika Kituo cha kimataifa cha mikutano AICC Mkoani Arusha. |
Vero Ignatus, Arusha.
Mkuu wamkoa wa Arusha Mrisho Gambo a meanza katika mkoa wa Arusha Kwa kuwawajibisha wbaadhi ya watendaji waliopo katika jiji Arusha katika ngazi mbalimbali
Ziara ambayo imeanza Jana Mkoani hapo Gambo amewataka watumishi wa idara mapato kumpa taarifa ya ukusanyaji wa kodi ya ardhi ndani ya wiki mbili .
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo ametoa ufafanuzi juu ya ukatwaji wa posho za madiwani katika Jiji la Arusha.
Ufafanuzi huo ameutoa katika kikao na watumishi wa Jiji la Arusha na
wadau mbali mbali katika ukumbi wa AICC katika siku yake ya kwanza ya
ziara kwa Jiji la Arusha.
"Hakuna haja ya kuwekeana vinyongo na nyinyi viongozi wenzangu kwani yote hayo yalifanyika kwa maslahi mapana ya taifa letu na wananchi wetu.....haiingii akilini kuona diwani mfano wa Kaloleni ama kata ya Kati kulipwa shilingi 80,000 kama posho ya nauli ilihali umbali anaokaa mpaka halmshauri hauzidi Kilometa mbili..." alinukuliwa alisema Mhe. Gambo.
"Na hili lilikua likifanyika kwa Jiji la Arusha pekee,ila pia maelekezo haya yalikwenda kwa halmashauri zingine za Ngorongoro na Arusha Vijijini kwani nao walikua na vitu vya namna,nimeona nitoe ufafanuzi kwani kumekua na dhana haya yanafanyika kwakua halmashauri ina madiwani wa Upinzani...la
hasha!!haya ni kutokana na mwelekeo wa serikali ya awamu ya tano chini
ya nahodha Mhe. Dr. John Magufuli inayohakikisha fedha za wanyonge
hazifujwi kwa maslahi ya wachache." Mhe Gambo aliongezea.
Ziara hiyo ya mkuu wa mkoa ni mwendelezo wa ziara zake katika wilaya za mkoa huo ambapo leo anaingia siku ya pili katika Jiji la Arusha.
Ziara hiyo ya mkuu wa mkoa ni mwendelezo wa ziara zake katika wilaya za mkoa huo ambapo leo anaingia siku ya pili katika Jiji la Arusha.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni