Mkurugenzi mwenza wa Tanzanite One,Faisal Juma pamoja na
viongozi wa serikali na wajumbe wa kamati ya shule ya Songambele
akikagua madarasa ambayo hayatumiki kutokana na nyufa baada ya shule
kukumbwa na mafuriko na kutangaza kujenga madarasa saba.
Mkurugenzi
mwenza wa Tanzanite One,Faisal Juma akizungumza katika mkutano na
wazazi wa shule ya msingi Songambele ambayo ina uhaba wa madarasa na
kutangaza kujenga madarasa saba Mwaka huu ili kupunguza tabu waipatayo
wanafunzi hao kwa kukoisa vyumba vya madarasa.
Na,Vero Ignatus .
Kampuni ya Tanzanite one imetangaza kujenga madarasa saba
baada ya kuripotiwa wanafunzi 1126 shule ya msingi Songambele iliyopo
Mererani wilaya ya Simanjiro kusoma katika madarasa manne .
Mkurugenzi
mwenza wa kampuni ya Tanzanite One,Faisal Shabhai amesema,kuwa baada ya
kuona kwenye vyombo vya habari shida ya madarasa katika shule
hiyo,wameamua kujitokeza kujenga shule hiyo.
Shabhai alisema,Tanzanite one kama mwekezaji Katika migodi
ya Tanzanite wanawajibu wa kusaidia masuala ya kijamii hasa kwa kuwa
wananufaika na madini ya Tanzanite.
"Tunajua tunawajibu wa kusaidia jamii hivyo tutajenga madarasa saba katika shule hii"alisema
Katibu Tawala wa wilaya ya Simanjiro,Zuwena Omar alishukuru kampuni Tanzanite One kwa msaada waliotoa kujenga madarasa hayo.
Omar alitoa wito kwa wawekezaji wengine waliopo Mererani kusaidia maendeleo ya Mererani.
Mwalimu Mkuu shule hiyo.Mwanahamisi Mussa alisema
wanakabiliwa na tatizo la uhaba wa madarasa, matundu 40 ya vyoo,Nyumba
za walimu na ofisi kwani wanafanyakazi chini ya miti.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni