Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya The Guardian Ltd,Jesse
Kwayu akiwaongoza washiriki wa warsha inayotolewa na Taasisi ya Vyombo
vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA-TAN) juu ya changamoto zilizopo
katika sheria mpya ya Huduma za Habari.
Baadhi ya Wanahabari kutoka mikoa ya Tanga,Arusha
,Manyara na Kilimanjaro wakishiriki katika warsha hiyo inayofanyika
katika Hoteli ya Impala jijini Arusha.
Mwandishi wa Habari wa Kituo cha Luninga cha ITV mkoa wa Manyara,Charles Masanyika akichangia jambo wakati wa warsha hiyo.
Mwandishi wa Habari wa Gazeti la Mwananchi mkoa wa Manyara ,Joseph Lyimo akichangia jambo katika warha hiyo.
Wakili Msomi na Mwanahabari mwandamizi James Marenga
akiwapitisha washiriki wa warsha hiyo katika vifungu mbalimbali vya
sheria ya Huduma ya Habari.
Mwandishi wa Habari Yusuph Mussa (kutoka mkoani Tanga) gazeti la Majira na VOA,akiguatilia Kwa makini mada zinazoendelea katika semina hiyo.
Afisa Habari na Utafiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari kusini mwa Afrika tawi la Tanzania (MISA-TAN) Sengiyumva Gasirigwa |
Mmiliki
wa Blog ya Vero Ignatus blog aliyevaa koti jeusi akifuatiwa na aliyeko
Julia kwake mwandishi wa gazeti la Tanzania Daima Mary Mwita
wakifuatilia mafunzo yanayoendelea.
Na.Murtadhwa Elbahsan, Dae es salaam.
Taasisi ya habari
kusini mwa Afrika(MISA-TAN) kwa kushirikiana na Shirika la Kijerumani
linaloshughulika na utawala bora la Friedrich Ebert Stiftung, wameandaa
semina kwa waandishi wa habari kuhusu sheria mpya ya Habari na
changamoto zinazotokana na sheria hiyo.
Semina hiyo
inafanyika katika Jiji la Arusha katika Hoteli ya Impala Jijini Arusha
na kuwashirikisha waandishi wa habari kutoka katika mikoa minne iliyopo
kanda ya Kaskazini.
Muwezeshaji katika semina hiyo
Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya The Guardian Ltd,Jesse Kwayu amesema kuwa
lengo kuu la warsha hiyo ni kuangalia changamoto zilizopo katika
sheria mpya ya Huduma za Habari.
Jesse anewataka
waandishi wa habari kila mmoja kuhakikisha kuwa anafanya kazi zake Kwa
usahaihi huku akiwataka kujiendeleza zaidi kielimu na kutoridhika na
kiwango cha elimu walichokuwa nacho.
Aidha semina hiyo
imewashirikisha baadhi ya waandishi wa habari kutoka katika mikoa ya
Tanga,Arusha ,Manyara na Kilimanjaro ambapo itafanyika Kwa Siku mbili.
Kwa
upande wake Wakili Msomi na Mwanahabari mwandamizi James Marenga
amefafanua baadhi ya vifungu mbalimbali vya sheria vya huduma ya habari
ambavyo amewataka wanahabari kuvifahamu Kwa undani zaidi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni