Msanii
Hussein Machozi ambaye sasa amerudi nchini kutoka nchini Italia
amefunguka na kusimulia kisa chake cha kufumaniwa alivyokuwa Kenya na
kusema kuwa kama asingekimbia huenda mambo yangekuwa mabaya kwake.
Hussein
Machozi amesema hayo kwenye kipindi cha Planet bongo ya East Africa
Radio na kudai kuwa yeye alikwenda Kenya kikazi na mtu ambaye alikuwa
anawasiliana naye alikuwa ni binti aliyeandaa show yake Kenya, hivyo
alipofika alimpokea Airport na kwenda naye hotel.
"Kwa
hiyo tulipofika hotel tulikuwa tunapanga mipango ya hapa na pale, kumbe
yule binti ana mshikaji wake ambaye ana wivu sana na yeye, hivyo yule
jamaa alikuja na magari kama mawili yakiwa na mabaunsa kibao.
"Wakatuzunguka
pale na kuanza kunipiga vibao ila nashukuru Mungu kuna baunsa mmoja
pale pale alinishtua na kuniambia nikimbie, hivyo niliruka ukuta wa
hotel na kukimbia.
"Kwa hiyo wale wahudumu pale ndiyo walianza kusambaza habari kuwa nimefumaniwa ila nisingekimbia huenda ingekuwa mbaya kwangu" alisisitiza Hussein Machozi
Mbali
na hilo Hussein Machozi anasema alimua kwenda nchini Italia baada ya
kuona muziki unampa mawazo hivyo Mungu akamfungulia mlango mwingine na
kuamua kusepa huko, ambako anadai anasoma na kufanya shughuli zingine
zinazomuingizia kipato.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni