Aidha,
kwenye mahojiano hayo Prof. Lipumba amesema kuwa amekuwa mstari wa
mbele kuhakikisha anaiongoza CUF katika kudai haki za wananchi tofauti
na Maalim Seif ambaye mara kadhaa ikitokea suala hilo haonekani akisema:
“Mwaka
2000 baada ya Uchaguzi Mkuu tuliingia kwenye maandamano Zanzibar,
lakini Maalim Seif alikwenda Uingereza nilikuwa mstari wa mbele.
Prof.
Lipumba amesema pia kuwa Maalim Seif amekuwa akidai kila anapokosana na
mtu kisiasa kuwa mtu huyo anatumiwa na CCM akitolea mfano wa Ahmad
Rashid, akisema:
“Ni kawaida ya Maalim Seif, akikosana na mtu kisiasa anasema anatumiwa na CCM. Rejea mgogoro na Ahmad Rashid".
Akizungumzia
kuhusu kumpokea na kumtambulisha kwa viongozi wa UKAWA aliyekuwa Waziri
Mkuu wa zamani wa Tanzania Edward Lowassa wakati anatoka CCM, Prof.
Lipumba alisema:
“Mbatia
ndiye aliyeniunganisha na Lowassa. Sikuwa na namba zake, na wakati
anakuja, nilisema wazi suala la rushwa ni mfumo siyo mtu.
“Mzigo mzito anapewa Mnyamwezi, lakini huu wa kumnadi Edward Lowassa ulinizidi uzito, nisingeweza kuubeba."
Wakai
huo huo Prof. Lipumba amebainisha kuwa hakuwa na nia ya kurejea katika
nafasi yake ya Uenyekiti wa CUF baada ya kujiuzulu, lakini aliombwa na
wanachama wa chama hicho.
“Sikuwa na nia ya kurudi kuwa Mwenyekiti CUF ila wanachama waliniomba nirudi baada ya uchaguzi kumalizika na hali kutulia”
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni