Waziri
Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa ametuma salamu za rambi rambi kutokana na
tukio la watu 32 kufariki dunia katika ajali ya basi.
Waliofariki katika ajali hiyo iliyotokea leo asubuhi Karatu, ni wanafunzi 29, walimu wawili, pamoja na dereva wa gari hilo.
“Nimepokea
kwa masikitiko taarifa ya ajali hiyo, ni ajali mbaya ambayo inaifanya
siku hii kuwa mbaya katika historia ya nchi yetu,”alisema
Miongoni mwa wanafunzi waliofariki ni pamoja na wanaume 11 na wasichana 18.
Kadhalika
maiti 32 zikiwamo za walimu wawili, dereva mmoja na wanafunzi 29
zimepokelewa sasa hivi katika Hospitali ya Lutheran Karatu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni