Wanafunzi
wa Shule wa Sekondari ya Arusha wakimsikiliza Mkufunzi kutoka Taasisi
ya Gemological Insitute of America (GIA) , Elizabeth Bokaba (hayupo
pichani). Wanafunzi hao wamepata mafunzo kuhusu mafunzo ya Jimolojia.
Wanafunzi
wa Shule ya Sekondari Arusha wakifuatilia mafunzo kwa vitendo kuhusu
elimu ya madini ya vito yanayopatikana chini, wakati wa Maonesho ya 6 ya
Kimataifa ya Madini ya Vito yanayoendelea jijini Arusha.
Mratibu
wa Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC), Eric Mpesa akiwaeleza jambo
wanafunzi wa Shule ya Sekondari Arusha wakati wa mafunzo ya Jemolojia
yaliyotolewa na Taasisi ya GIA wakati wa Maonesho ya 6 ya Kimataifa ya
Vito Arusha yanayoendelea jijini Arusha.
Mkufunzi
kutoka Taasisi ya Gemological Institute of America (GIA),
Elizabeth Bokaba, akiwafundisha elimu ya Jemolojia wanafunzi wa Shule
ya Sekondari Arusha.
Wanafunzi
wa Shule ya Sekondari Arusha wakiangalia madini ya Tanzanite katika
Banda la Kampuni Gliters Gems Limited wakati walipotembelea mabanda ya
maonesho baada ya kupata mafunzo ya Jemolojia.
Mfanyabiashara
wa Madini wa Kampuni ya Abdulhakim Mulla akiwaonesha wanafunzi wa Shule
ya Sekondari Madini ya Tanzanite. Mulla alitumia nafasi hiyo
kuwafundisha tofauti ya madini yaliyonakishiwa na ambayo bado
hayajakatwa.
Jumla
ya Wanafunzi 55 kutoka Shule za Sekondari za Arusha Day, Arusha
Sekondari na Wining Sprit wenye umri kati ya miaka 12- 15 wamepatiwa
mafunzo ya Jemolojia katika Maonesho ya 6 ya Kimataifa ya Madini ya Vito
yanayoendelea jijini Arusha.
Mafunzo
hayo yanayojulikana kama GemKids yametolewa na Wakufunzi kutoka
Taasisi ya Gemological Institute of America (GIA) na kuratibiwa na Kituo
cha Jimolojia Tanzania Cha Arusha, (TGC).
Akizungumzia
umuhimu wa mafunzo hayo, Mratibu wa TGC, Erick Mpesa amesema kuwa,
mafunzo hayo ya Jemolojia, yanalenga kuwapa ufahamu wanafunzi ili kuwa
na uelewa wa madini ya vito, kujua matumizi yake, kuyatumia na baadaye
kuwawezesha kuingia katika biashara ya madini huku wakiwa na uelewa
mzuri na rasilimali hizo ambazo zinapatikana katika maeneo mbalimbali
nchini.
Akizungumzia
mahusiano ya TGC na Taasisi ya GIA, Mpesa amesema kuwa, TGC imelenga
kuendeleza ushirikiano na Taasisi hiyo kwa siku za baadaye hususani
katika masuala ya utafiti na mafunzo na kuongeza kuwa, uhusiano uliopo
baina ya taasisi hizo, umewezesha baadhi ya watumishi wa kituo hicho
kupata mafunzo katika taasisi hiyo.
Kuhusu
mpango wa TGC kutoa mafunzo kwa Watanzania, alisema kuwa, tayari
kupitia Maonesho ya Vito ya Arusha, kituo hicho kuanzia mwaka 2014
kimetoa mafunzo ya ukataji na unga'rishaji wa madini ya vito kwa jumla
wanawake 47 na kueleza kuwa, hivi sasa jumla ya wanawake 18 wanaendelea
na mafunzo hayo na wanatarajiwa kuhitimu ifikapo tarehe 19 ya mwezi
huu.
"Kutokana
na changamoto ya ajira wahitimu wetu tunawashauri kujiunga katika
vikundi ili kuwawezesha kupata ruzuku pale zinapotolewa na Serikali. Hii
inawezesha rasilimali inayotumika kuwafundisha kuwawezesha vijana hawa
isipotee bure. Lengo letu ni kuwawezesha waweze kujiajiri na kuajiriwa,"
alisisitiza Mpesa.
Maonesho ya 6 ya Kimataifa ya Vito ya Arusha yalianza rasmi tarehe 3 Mei na yanataajiwa kufungwa tarehe 5 Mei,2017
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni