Wanaume 11 ambao ni raia wa Tanzania wamekamatwa na Polisi na kufikishwa Mahakamani wiki hii Johannesburg Afrika Kusini .
Radio
na Mtandaoni Johannesburg wiki hii kumeripotiwa kuwa kosa lililofanya
Wanaume hao 11 kukamatwa na Polisi ni kumbaka Mwanamke mjamzito mwenye
umri wa miaka 22 aliyekua akitoka kazini saa kumi na moja alfajiri.
Mwanamke
huyo alikua akitoka kazini na Mfanyakazi mwenzake ambaye ni Mwanaume
ambapo ghafla walivamiwa na kundi la Wanaume wenye silaha za moto na
wakamvuta Mwanamke huyo kabla ya kumpiga Mfanyakazi mwenzake ambae
baadae alifanikiwa kutoroka.
Baada
ya Mfanyakazi huyo kutoroka aliwapigia simu Polisi na wakafanikiwa
kuwahi eneo la tukio na kukuta Wanaume hao wakimbaka kwa zamu Mwanamke
huyo mwenye ujauzito wa miezi mitatu.
Polisi
wapatao kumi waliingia kwenye jengo tukio lilikofanyika na kumuokoa
Mwanamke huyo aliyekua kwenye hali mbaya ambapo walimpeka Hospitali huku
Watuhumiwa wakichukuliwa na kupandishwa Mahakamani siku ya Jumatano.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni