Bilionea
wa nyumba za Lugumi aliyeteka vichwa vya habari siku za hivi karibuni,
Dk. Louis Shika, amekamilisha malipo ya bima kwa ajili ya kutumiwa fedha
zake kutoka nchini Urusi..
Dk.
Shika aliingia matatani baada ya kushinda mnada wa uuzwaji wa nyumba za
Said Lugumi hali iliyosababisha kukamatwa na polisi, lakini binafsi
alisisitiza kuwa fedha hizo anazo na sasa anaelekea kuthibitisha hilo
kwa kufanya mchakato wa kutumiwa fedha.
Waandishi
wa habari walimkuta Dk. Shika akiwa katika huduma za mtandao wa
internet katika shirika la Posta Jijini Dar es Salaam, ambao walikuwa
katika ziara ya Naibu Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi, Mhandisi
Atashasta Nditiye na kujikuta hata mwenyewe akimshangaa bilionea huyo.
Akizungumza
na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza kutuma taarifa za miamala
hiyo, Dk. Shika amesema ametuma kiasi cha dola 100 ambapo anatarajia
muda si mrefu ataweza kutumiwa fedha zake na kwenda kulipia asilimia 25
ya fedha zinazotakiwa katika nyumba hizo.
Alipoulizwa
kama fedha hizo zikichelewa na kukuta mchakato huo wa malipo umepita,
amesema kwa kujiamini, atanunua nyingine kwani Dar es Salaam kuna nyumba
nyingi zinazouzwa siyo lazima hizo za Lugumi.
Kiasi
hicho cha fedha, amekilipa kwa kwa Benki ya Equity kwenda Benki ya
Bankok nchini Thailand, mchakato utakaomwezesha kutumiwa fedha zake na
kuweza kununua nyumba hizo.
Katika
hatua nyingine Dk. Shika alisifia huduma za shirika hilo na kueleza
kwamba ndiyo hutuma huduma za internet katika kutuma nyaraka zake
mbalimbali ndani na nje ya nchi.