TAHADHARI
BAKORA ZITAKUHUSU
Kama wewe ni kijana wa kiume usisimame na wanafunzi wa like, ukionekana tu utachapwa viboko 12 au faini Tshs. 10,000
Ukiwa katika kata ya Ihungwe wilayani Sengerema usithubutu kusimama na mwanafunzi wa kike, ukikamatwa utachapwa viboko 12 au faini ya 10,000 baada ya viongozi wa kata hio kupitisha rasmi sheria hio katika kikao chao cha baraza la maendeleo ya kata kilichofanyika hivi karibuni, kufuatia tatizo la kupata mimba wanafunzi wa kike kuzidi kuwa sugu.
Sheria hio ndogo imepitishwa ikitanguliwa na agizo la Mkuu wa wilaya ya Sengerema Nd. Emanuel Kipole alieagiza Wanaume watakaokutwa na wanafunzi wa kike wapigwe bakora 12 au faini ya Tsh.10,000, agizo hilo alilitoa mwezi oktoba mwaka 2017
Chanzo: Gazeti la Mwananchi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni