CHAMA CHA SKAUTI TANZANIA CHAELEKEA KWENYE UCHAGUZI MKUUMAPEMA MWAKA HUU 2018.
Habari na, Murtadhwa Elbahsan.
Chama cha Skauti Tanzania kimetangaza upatikanaji wa fomu za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi, hii ni desturi ya upatikanaji wa uongozi wa Skauti Tanzania.
Kwa kupitia Mkutano Mkuu Maalum wa Baraza Kuu la Chama cha Skauti Tanzania, ambacho ndicho chombo kincho piga kura na kupata viongozi WA juu wa chama hicho, Baada ya kukamilisha mhakato wa upatikanaji wa majina 3 ya skauti mkuu yatakayo pelekwa kwa Mlezi wa Skauti Tanzania ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuteua Skauti Mkuu.
"Kwa sasa chama cha skauti Tanzania kinataraji kufanya uchaguzi mkuu wa kupata viongozi wao wa juu, ambapo tarehe rasmi za uchaguzi huo ni 22 Februari 2018 katika ukumbi wa Karimjee" alisema Bi. Eline Kitaly ambaye ni Kamishna Mtendaji wa Skauti
Fomu rasmi ya kugombea nafasi ya skauti Mkuu hii hapa chini......
"Kwa sasa chama cha skauti Tanzania kinataraji kufanya uchaguzi mkuu wa kupata viongozi wao wa juu, ambapo tarehe rasmi za uchaguzi huo ni 22 Februari 2018 katika ukumbi wa Karimjee" alisema Bi. Eline Kitaly ambaye ni Kamishna Mtendaji wa Skauti
Fomu rasmi ya kugombea nafasi ya skauti Mkuu hii hapa chini......
VIGEZO MAALUM VYA KUMPATA SKAUTI MKUU
Mwombaji awe na sifa zifuatazo:1. Awe na umri usiopungua miaka 45
2. Awe kiongozi aliyewahi kutoa huduma iliyotukuka kwa
Chama cha Skauti Tanzania na Jamii
3. Awe na ueledi wa mambo ya Skauti
4. Awe miongoni mwa Wakufunzi Wasaidizi (ALTs)
5. Awe na uzoefu usiopungua miaka 15 katika uongozi wa
Skauti Watu Wazima (Adult in Scouting)
6. Awe na Uwezo wa kusimamia na kuendeleza Skauti kwa
ujumla
Eidha kwa sasa Bi. Mwantum B. Mahiza ndio Skauti Mkuu na Kamishna Mkuu wa Skauti ni Ndugu Abdulkarim E. H. Shah.
Chama cha Skauti pamoja na kuwa na Makamishna wakuu wa saidizi pia kuna Naibu Kamishna Mkuu ambaye ni ndugu Rashid K. Mchatta, viongozi wote hao wanamaliza muda wao wa uongozi tangu kuchaguliwa kwaomara baada ya kupatikana viongozi wapya baada ya uchaguzi na kfuatiwa kuteuliwa kwa Skauti Mkuu na Mlezi wa Skauti (Rais wa nchi)
Kipenga cha kumtafuta Skauti Mkuu kimepulizwa, nafasi ziko wazi na mwisho wa kurudisha fomu ni tarehe 15 Januari, 2018 waweza kujaza fomu kielektronik kwa kubonfya hapa >>>>> https://tzcentenary2017.wordpress.com/2018/01/06/fomu-ya-uongozi-chama-cha-skauti-tanzania/ thttps://www.scout.org/tanzania pia waweza kupata fomu ya uongozi kwa barua pepe ya: szone2012@live.com au dsmscout@gmail.com
Waweza pia kupakua fomu hii kwa https://web.facebook.com/SCF360
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni