Ofisa
wa Jeshi la polisi mstaafu Mashaka Mdachi (72) amefikishwa Mahakama ya
Hakimu Mkazi mkoa wa Morogoro kujibu shitaka la kumbaka na mwanafunzi wa
darasa la tano mwenye miaka 13.
Mbele
ya hakimu wa mahakama hiyo Elizabert Nyembele, mwanasheria wa Serikali
Mary Lundu alidai mshtakiwa alitenda kosa hilo kati ya Januari 2017 na
Oktoba 2018 katika nyakati tofauti huko Area Five kata ya kichangani
Manispaa ya Morogoro.
Mwanasheria
huyo alidai mahakamani hapo Ijumaa ya Novemba 23, 2018 kuwa mshtakiwa
alifanya kitendo hicho huku akijua ni kosa kisheria na kumuathiri
kisaikolojia binti huyo.
Alipotakiwa
kujibu shitaka hilo mshtakiwa huyo alikana na mahakama Iliahirisha kesi
hadi Desemba 6, 2018 itakapotajwa tena wakati polisi wakiendelea na
upelelezi wa kesi hiyo na mshtakiwa alipelekwa rumande baada ya kukosa
wa kumdhamini.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni