Na. Vero Ignatus, Manyara
Jeshi
la polisi Mkoani Manyara, linawashikilia watu watatu kwa kudaiwa
kukutwa na nyara za serikali ikiwemo vipande vitatu vya jino la Tembo.
Kamanda
wa polisi wa mkoa wa Manyara, Augostino Senga akizungumza jana alisema
watu hao walikamatwa kwenye nyumba ya kulala wageni ya Top In One
iliyopo mtaa wa Oysterbay mjini Babati.
Kamanda
Senga aliwataja watu hao kuwa ni Anthony Paschal (28) na Juma Ingi wote
wakazi wa Endasak wilayani Hanang' na Tluway Gosi mkazi wa Simbay
wilayani Hanang'. Alisema mbinu waliyotumia ni kuficha vipande hivyo
ndani ya mfuko wa sulphate kisha kuweka chini ya uvungu wa kitanda ili
wakaiuze.
Alisema
baada ya timu ya makachero kwa kushirikiana na maofisa wanyamapori wa
shirika la hifadhi ya Taifa ya Tarangire kupata taarifa walifika eneo
hilo na kuwakamata watu hao. "Watuhumiwa hao wote wanashikiliwa na
polisi na tunaendelea na upelelezi kabla ya kuwafikisha mahakama kwa
ajili ya kujibu mashtaka yanayowakabili," alisema kamanda Senga.
Katika
tukio lingine, kamanda Senga alisema watu watatu wanashikiliwa na
polisi kwa tuhuma za kukutwa na lita 40 za pombe haramu ya moshi maarufu
kama gongo. Alisema watu walikamatwa juzi kwenye kijiji cha Kazamoyo
kata ya Kisangaji wilayani Babati wakiwa wamebeba kwenye pikipiki aina
ya Skygo yenye namba za usajili MC 970. Aliwataja watu hao kuwa ni
Daniel Hewasi (47) mkazi wa Magugu, Hussein Athuman (50) mkazi wa kijiji
cha Kazaroho na Idd Hamis (35) mkazi wa kijiji cha Magugu.
Alisema
watu hao walikuwa wamebeba pombe hiyo haramu kwenye pikipiki hiyo
wakiwa wamehifadhi kwenye madumu mawili ya lita 20 kila moja.Alisema
pikipiki hiyo iliyokuwa imebeba pombe hiyo haramu ni mali ya Idd Hamis
na lengo lao ilikuwa ni kwenda kuuza ili kujipatia kipato.
Alisema polisi wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo kabla ya kuwafikisha mahakamani wakajibu mashtaka yanaoyowakabili.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni