Mamlaka
ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii SSRA, kupitia
Mkurugenzi Mkuu, Irene Isaka, imekanusha malalamiko ya kupunguzwa kwa
mafao ya wastaafu kupitia kanuni mpya za mwaka 2018 na kudai kuwa,
taratibu zinazotumika ni za mwaka 2014.
Akizungumza
na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam, Irene Isaka amesema
changamoto hiyo inasambazwa na wanachama wachache, pia ni jambo ambalo
linaweza kuzungumzika na kuongeza kuwa sheria ambayo imepitishwa
inalenga kuifanya mifuko hiyo pamoja ili ilete faida kwa wanachama wake.
“Sheria
ya kuunganisha mifuko imeleta usawa wa wanachama, kwa viwango
wanavyochangia, kupunguza gharama za uendeshaji, jambo lingine ni kuweka
uwaniano kati ya wachangiaji na wastaafu, lakini sasa tuna uwiano
mzuri, pia sasa hivi hata akifariki mafao yataendelea kwa miaka 3,”
amesema Kisaka.
Isaka
ameeleza kuwa, haikuwa sahihi kundi dogo kulipwa mkupuo mkubwa wa zaidi
ya mara tatu ya michango aliyochanga kwa kipindi chote cha ajira yake
tofauti na wenzao hivyo, asilimia 25% iliyopunguzwa kwenye mkupuo
imewekwa kwenye pensheni ya kila mwezi ambayo imeongezeka kwa asilimia
50%.
“Sheria
hii imetatua changamoto, kwa hiyo niwaondoe wasiwasi lengo ni zuri na
hata wanaolalamika ni wachache kwa sababu tunawastaafu zaidi ya laki
moja kwa hiyo ni sehemu ndogo ya wanachama wenye hofu,” ameongeza.
“Kuhusu
wategemezi wameshalipwa wengi, kwa sheria mpya imeongeza mafao na
maslahi kwa wanachama wetu, ndiyo maana watu wengine kutoka nchi za
Burundi, Namibia wamekuja kujifunza kwetu kwa sababu tumefuata vizuri
kanuni za shirika la kazi duniani 'ILO'.”
Novemba
22 mwaka huu, Mbunge wa Bunda, Ester Bulaya alisema “tuliwaambia
dhamira ya kuunganisha mifuko ya hifadhi ya jamii ilikuwa ni serikali
kukwepa madeni inayodaiwa na mifuko ya hifadhi ya jamii ambayo kwa sasa
inafikia trilioni 8 kwa sababu waliwekeza kwenye miradi isiyokua na
tija,”
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni