Na Rhoda Ezekiel Kigoma,
KAMATI ya ulinzi na Usalama Wilayani Kasulu
imeteketeza Shamba la bhangi hekari moja iliyo kuwa ikilimwa katika
hifadhi ya poli la Akiba Makere Kusini pamoja na kukamata Watuhumiwa
wanne wawili wakiwa ni raia wa Burundi wakiwa wanatumiwa katika Kilimo
cha hicho.
Akizungumza na waandishi wa habari Kaimu Mkuu wa
wilaya ya Kasulu ambae pia ni Mkuu wa Wilaya ya Buhigwa Kanali Marko
Gaguti wakati wa kuteketeza shamba hilo alisema kumekuwa na tabia ya
wakulima wengi kulima bhangi pembezoni mwa mji wakichanganya na mazao
Mengine suala linalopelekea watoto wengi kuharibika na uharifu
kuongezeka.
Gaguti alisema baada ya kupokea taarifa kutoka kwa
Wananchi kwamba kuna mtu analima bhangi jeshi la polisi kwa kushirikiana
na kamati ya ulinzi na usalama ilifanya msako na kukamata shamba la
Mkulima, Yotham Ngeze aliekuwa akiwatumia vibarua wanne wakiwemo warundi
wawili na vijana wawili ambao walikuwa wakilima shamba hilo.
Aidha Gaguti aliwataka wakulima kuacha tabia ya
kulima bhangi zao ambalo ni haramu na badala yake watumie aridhi nzuri
waliyo nayo kulima mazao ya chakula kutokana na hali ya upatikanaji wa
chakula ulivyo kwa sasa, na kwa atakae kutwa analima zao hilo hatua za
kisheria zitachukuliwa dhidi yake Serikali inamacho mengi wataendelea
kuwafuatilia popote pale .
Pia Mkuu huyo aliwataka Wakulima kuacha tabia ya
kuwatumia Wahamiaji haramu katika mashamba yao hali inayo sababisha
Migogoro ya Wakulima kuongezeka kutokana na ugomvi unaotokea baada ya
kuwatumia vibarua hao na kuacha kuwalipa, kulikuwa na kesi nyingi za
raia kutoka Burundi kuwauwa watanzania kwa kuwalipizia kisasi baada ya
kuwatumia bila malipo.
"Niwaombe wakulima Muachane na tabia ya kuja kulima
bhangi katika hifadhi zetu za misitu uhalifu umekuwa ukiongezeka kila
siku ni kutokana na Vijana wanapo tumia madawa ya kulevya wengi wao
huishia kufanya uhalifu na wengine
kushindwa kuendelea na masomo hatutavumilia watoto wetu na Wananchi
waendelee kuteseka tutakae Mkamata atalipa faini na kifungo pia",alisema
Gaguti.
Kwa upande wake Kamanda Wa jeshi la polisi Mkoa wa
Kigoma DCP Fredinandi Mtui alisema kwa Kipindi cha mwezi mmoja huu wa
tatu walikamata hekari saba za bhangi na watuhumiwa nane, ambapo hekari
sita ziliteketezwa katika Wilaya ya Kakonko na Hekari moja katika Wilaya
ya Kasulu na jeshi la polisi linaendelea na kuwasaka wote wanao lima na
kutumia bhangi ilikuweza kukomesha madawa ya kulevya.
Nae Mmiliki wa shamba la bhangi katika msitu wa
hifadhi Makere Yotham Ngeze alikili kulima zao hilo na kwamba analima
kwaajili ya matumizi yake binafsi na kwamba anapo tumia bhangi anajikuta
anafanya kazi kubwa sana ya kulima kwa siku anaweza kulima nusu heka
akiwa amwtumia zao hili.
Alisema alianza kutumia bhangi tangu mwaka 1973 akiwa
katika Mashamba ya Mikonge Mkoani tabora na amekuwa akilima zao hilo
liweze kumsaidia kupata bhangi kwa urahisi kutokana na mazoea aliyo
jiwekea tangu akiwa kijana hawezi kuishi bila bhangi.
Nao baadhi ya vijana waliokuwa wakimlimi0a mzee huyo
akiwemo Simoni Ndayahimana raia wa Burundi wamejikuta wakianza matumizi
ya bhangi baada ya kulima katika shamba hilo hali inayopelekea vijana
wengi kupoteza nguvu kazi kutokana na matumizi na ulimaji wa madawa ya
kulevya.
Kaimu
Mkuu wa wilaya ya Kasulu ambae pia ni Mkuu wa Wilaya ya Buhigwa Kanali
Marko Gaguti akishiriki kuteketeza bhangi iliyokuwa imelimwa huku ikiwa
imechanganywa na mazao mengine
Zoezi la kuteketeza Bhangi likindelea
Baadhi ya Watuhumiwa waliokamatwa wakiohojiwa na
vyombo vya habari kufuatia kukamatwa kwa tuhuma za kulima Bhangi katika
hifadhi ya poli la Akiba Makere Kusin,
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni