Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Uhifadhili
Mahotelini na Majumbani kwa Huduma za Jamii na Ushauri (CHODAWA), Said
Wamba akizungumza na waandishi wa habari wakati kongamano na baadhi ya
matawi ya vyama wafanyakazi Dar es Salaam. (PICHA NA DALILA SHARIF)
Na Dalila Sharif
KATIBU Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Uhifadhili
Mahotelini na Majumbani kwa Huduma za Jamii na Ushauri (CHODAWA), Said
Wamba amezitaka Sekta za wafanyakazi zisizorasmi kujiunga kwa kuanzisha
vyama vya wafanyakazi na taasisi binafsi ili kuweza kulinda na kutetea
maslahi yao.
Akizungumza na waandishi wa habari katika kongamano hilo la
matawi ya vyama vya wafanyakazi (CHODAWO), Jijini Dar es Salaam leo
alisema umuhimu wa vyama vya wafanyakazi ni kusaidia kulinda na kutunza
maslahi ya wafanyakazi na wafanyabiashara ndogondogo.
Alisema wafanyakazi wengi na wafanyabiashara nchini
wamekuwa hawajui kusimamia haki zao na kukabiliana na matatizo
yanayowakabili katika shughuli zao za kukuza uchumi wa Taifa hilo.
“Wafanyakazi na wafanyabiashara wanatakiwa kuunda vyama kwa
lengo la kuweza kuwatatulia matatizo yanayowakabili wanapokuwepo kazini
na kukabiliwa na majanga au kudai haki ya kazi zake endapo amedhulumiwa
, chama kinauwezo mkubwa wa kuwasilisha changamoto zao,”alisema Wamba.
Mratibu wa Shirikisho wa (CHODAWA) Vicky Kanyoka alisema
kuwa wafanyakazi wanawake wa majumbani wa haki ya kusimamiwa haki zao
katika kuwatetea na kuwasehea hivyo wapo baadhi ya waafanyabiashara
wanawake hufanya kazi na kuanzisha baisahara bila kuwa na vyama na
kushindwa kusimamia haki zao.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni