Kwamba
tarehe 23.04.2017 majira ya 18:45hrs jioni katika mtaa wa mkuyuni
sokoni kata ya mkuyuni wilaya ya nyamagana jiji na mkoa wa mwanza, mtu
mmoja mwanamume aliyrfahamika kwa jina la faraja anselem miaka 31, mkazi
wa mtaa wa mkuyuni sokoni, alikutwa akiwa amejinyonga chumbani kwake
hadi kufariki dunia kwa kutumia kamba ya katani aliyokua ameifunga
kwenye paa la chumba, kitendo ambacho ni kosa kisheria.
Inasemekana kuwa taraehe tajwa hapo juu marehemu alibaki
mwenyewe nyumbani, aidha inadaiwa kuwa kabla ya kufanya tukio hilo
marehemu alionekana akiingia chumbani kwake kisha akafunga mlango ndipo
baada ya muda kupita watoto waliokua wakicheza maeneo hayo waliona miguu
ikining’inia dirishani ndipo walitoa taarifa kwa wazazi wao.
Majirani baada ya kuona tukio hilo walitoa taarifa polisi,
ambapo askari walifanya ufuatiliaji wa haraka hadi eneo la tukio na
kuukuta mwili wa marehemu ukining’inia mahali hapo, mwili wa marehemu
umehifadhiwa hospitali ya rufaa ya bugando kwa ajili ya uchunguzi pindi
uchunguzi ukikamilika utakabidhiwa kwa ndugu wa marehemu kwa ajili ya
mazishi. Aidha upelezi kuhusiana na kifo hicho bado unaendelea.
Kamanda wa polisi mkoa wa mwanza naibu kamishina wa polisi
ahmed msangi anatoa wito kwa wakazi wa jiji na mkoa wa mwanza, akiwaomba
kuwa pale watakapoona mtu amekuwa na msongo wa mawazo kwa muda mrefu
hadi inapelekea kuweza kufanya kitu kisicho cha kawaida cha kuweza
kujidhuru yeye mwenyewe au watu wengine, wamfikishe kwa wataalamu wa
ushauri nasaha ili waweze kumshauri na kumwaondoa katika hali hiyo ya
msongo wa mawazo na kisha kurudi katika hali ya kawaida na kuweza
kuendelea na maisha.
Katika tukio la pili,
Kwamba tarehe 23.04.2017 majira ya saa 14:33hrs katika mtaa
wa kiloleli kata ya nyamanoro wilaya ya ilemela jiji na mkoa wa mwanza,
askari wakiwa doria na misako walifanikiwa kumkamata mtu aliyefahamika
kwa jina la donatus sebastina miaka 16, mkazi wa kiloleli akiwa na pombe
iliyeowekwa kwenye vifunganishio vya plastiki almaarufu viroba aina ya
empire pakiti 103, kitendo ambacho ni kosa kisheria.
Awali askari wakiwa kwenye doria na misako walipokea
taarifa kutoka kwa wasiri kwamba maeneo tajwa hapo juu yupo mtu
anayefanya biashara ya kuuza pombe ya viroba kwa siri, kutokana na
taarifa hizo askari walifanya upelelezi wa kimyakimya huku wakiendelea
na doria ndipo baada ya muda waliweza kufahamu mahali anapoishi
mtuhumiwa na kufanikiwa kumkamata akaiwa na pakiti 103 za pombe
iliyohifadhiwa kwenye vifungashio vya plastiki almaarufu viroba aina ya
empire.
Mtuhumiwa yupo katika mahojiano na polisi, pindi uchunguzi
ukikamilika atafikishwa mahakani, aidha upeleezi na misako ya kuwatafuta
watu wengine wanaojihusisha na biashara hiyo ya pombe za viroba bado
unaendelea.
Kamanda wa polisi mkoa wa mwanza naibu kamishina wa polisi
ahmed msangi anatoa wito kwa wakazi wa jiji na mkoa wa mwanza akiwataka
kuendelea kutoa taarifa mapema kwa jeshi la polisi ili watu
wanaojihusisha na biashari hiyo ya pombe za viroba waweze kukamatwa na
kifikishwa katika vyombo vya sheria.
Imetolewa na:
Dcp: Ahmed Msangi.
Kamanda wa Polisi (m) Mwanza
Kamanda wa Polisi (m) Mwanza
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni