Mabalozi wakiwa Bandarini tayari kwa safari ya kuelekea Zanzibar kwenye uzinduzi wa RSA Zanzibar. |
Na. Murtadhwa Elbahsan, Dar es saalm
Viongozi wa RSA wafunga safari kwenda kuzindua RSA Zanzibar leo tarehe 18/04/2017. Msafara huo ukiongozwa na DCP Mohammed Mpinga (Mlezi wa RSA Tanzania) pamoja Mwenyekiti wa RSA Nd.John Seka
Baada ya miaka 3 ya RSA Tanzania Bara, leo hii RSA itazinduliwa rasmi huko Tanzania Visiwani (Zanzibar) kwa lengo la kukuza taasisi lakini pia kuwafikia watanzania wote ili kuwa chachu ya kuondoa ajali nchini, RSA imekua ikijikita katika utoaji wa elimu za usalama barabarani lakini pia kuhusu masuala ya bima, kwa wamiliki wa vyombo vya moto na watumiaji wa vyombo vya moto (Abiria).
Mapema leo hii RSA itazinduliwa rasmi Visiwani Zanzibar na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanziba Mh. Balozi Seif Ally Iddi, katika ukumbi wa Baraza la wawakilishi Unguja. Sherehe hizo za uzinduzi zitafnyika kuanzia Saa sita mchana leo hii.
DCP Mohammed Mpinga (lezi wa RSA) akiwa na Viongozi wa RSA Taifa kwenye Boti wakielekea Zanzibar kwaajili ya uzinduzi wa RSA. |
Mabalozi wakibadilishana mawazo wakati wa safari ya kuelekea Zanzir |
Mabalozi wakiwa ndani ya boti wakielekea Zanzibar |
Mabalozi wakiwa ndani ya boti wakielekea Zanzibar |
>>>>> Tujikumbushe
RSA ni kifupi cha maneno ROAD SAFETY AMBASSADORS ikiwa na maana Mabalozi wa Usalama Barabarani. Motto wa RSA: "USALAMA BARABARANI NI HAKI NA JUKUMU LETU SOTE"
Taasisi hii ilianzishwa 17.12.2013. Malengo ya RSA kwa ujumla ni:
1. Kufanya kazi kama trafiki jamii kwa kuripoti matukio yote ya uvunjifu wa sheria za babarani.
2. Kutoa elimu kwa umma kuhusu usalama barabarani
3. Kuelimishana RSA kwa RSA kuhusiana na masuala mbalimbali yahusuyo usalama barabarani na bima
4. Kuwa chachu ya mabadiliko ya sera, sheria za usalama barabarani, mienendo na tabia za askari na madereva barabarani.
5. Kuwa mfano wa kuigwa(balozi) wa kutii bila shuruti sheria na taratibu za Usalama barabarani.
6. Kushirikishana uzoefu kutoka mahali mbalimbali duniani kuhusu usalama barabarani.
7. Kutumia majukwaa ya RSA kama sehemu ya kuuliza maswali, kujibu maswali, na kujadili masuala mbalimbali yahusuyo usalama barabarani.
8. Kupeana taarifa mbalimbali kuhusiana na usalama barabarani na hali ya barabara.
Taasisi hii inamakundi yaliyopo whatsapp yanayoitwa RSA-KULIKONI BARABARANI.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni