Msanii
Rutyfiya Abubakary maarufu kama ‘Amber Ruth’ na mpenzi wake Said Bakary
Kitomali wamekosa tena dhamana kwa mara ya tatu katika kesi
inayowakabili ya kufanya mapenzi kinyume na maumbile.
Mbali
na Amber Ruth na Said Bakary, mshtakiwa mwingine ni James Charles
maarufu kama ‘James Delicious’ ambaye yeye yupo nje kwa dhamana.
Mshtakiwa
Amber Rutty alimueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Augustine, Rwezire kuwa
mdhamini wake mmoja amefika mahakamani hapo lakini mwingine bado
hajafika.
Baada
ya kueleza hayo, Hakimu Rwezire amemwambia Amber Rutty kwamba dhamana
ipo wazi na shughuli za mahakama zinaisha saa 9 alasiri hivyo wadhamini
wake wakikamilika atadhaminiwa.Kesi imeahirisha hadi December 10,2018.
Katika
kesi hiyo kosa la kufanya mapenzi kinyume na maumbile linamkabili Amber
Ruth, ambapo anadaiwa amelitenda kati ama baada ya October 25, 2018
ambapo alimruhusu Said Bakary kumuingilia kinyume na maumbile, kosa
ambalo amelikana.
Pia
kosa jingine la kufanya mapenzi kinyume na maumbile, linamkabili
mshtakiwa wa pili Said Bakary ambapo anadaiwa kati ama baada ya October
25,2018 jijini Dar es Salaam alifanya mapenzi na Amber Rutty kinyume na
maumbile ambapo alisema si kweli.
Kosa
la tatu la kuchapisha video ama picha za ngono, ambapo linamkabili
James Charles ama James Delicious akidaiwa kati ya October 25,2018
alisambaza video za ngono kupitia magroup ya Whatsapp.
Kosa
jingine la nne ni kusababisha kusambaa picha za ngono linamkabili Amber
Ruth na Said Aboubakary ambapo wanadaiwa kati October 25,2018
walisababisha kusambaza picha za ngono kupitia makundi ya Whatsapp. Kosa
ambalo wamesema si kweli.
Ili
Amber Rutty na mpenzi wakewadhaminiwe wanatakiwa kutimiza masharti
ya kuwa na wadhamini 2 ambapo kila mtu atasaini bondi ya Shilingi
Milioni 1
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni