Powered by: Elbahsan Web & Blog Designer
Ijumaa, 28 Aprili 2017
Vyeti Feki: Rais Maguli Afuta Zaidi ya Ajira Elfu 9 Za Walioghushi Vyeti
Rais
Dk. John Pombe Magufuli, ameiagiza Wizara ya Fedha kufuta mara moja
ajira za watumishi wa umma 9,932 waliobainika kughushi vyeti, kwenye
orodha ya malipo ya watumishi wa umma.
Akiongea leo mara baada ya kupokea ripoti ya uhakiki wa vyeti vya watumishi wa umma mjini Dodoma, Rais Magufuli pia amewataka watumishi hao kuondoka wenyewe na iwapo watakaidi wakamatwe na vyombo vya dola na kushtakiwa.
Rais Dk. Magufuli pia ameziagiza mamlaka husika kujumuisha nafasi 9,932 za ajira ambazo zimeachwa wazi na watumishi wa umma walioghushi vyeti, kwenye ajira mpya zaidi ya elfu 52 za serikali ili ziweze kuchukuliwa na watu wenye sifa na uwezo wa kumudu nyadhifa zilizoachwa.
Akizungumza wakati akiwasilisha ripoti hiyo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Angela Kairuki, amesema, kwa Mujibu wa Kanuni na Sheria za nchi zinabainisha wazi kuwa mtu atakaebainika kughushi vyeti au kutoa taarifa za uongo adhabu yake ni pamoja na kifungo cha Jela.
Akiongea leo mara baada ya kupokea ripoti ya uhakiki wa vyeti vya watumishi wa umma mjini Dodoma, Rais Magufuli pia amewataka watumishi hao kuondoka wenyewe na iwapo watakaidi wakamatwe na vyombo vya dola na kushtakiwa.
Rais Dk. Magufuli pia ameziagiza mamlaka husika kujumuisha nafasi 9,932 za ajira ambazo zimeachwa wazi na watumishi wa umma walioghushi vyeti, kwenye ajira mpya zaidi ya elfu 52 za serikali ili ziweze kuchukuliwa na watu wenye sifa na uwezo wa kumudu nyadhifa zilizoachwa.
Akizungumza wakati akiwasilisha ripoti hiyo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Angela Kairuki, amesema, kwa Mujibu wa Kanuni na Sheria za nchi zinabainisha wazi kuwa mtu atakaebainika kughushi vyeti au kutoa taarifa za uongo adhabu yake ni pamoja na kifungo cha Jela.
Wakuu wa Mikoa, Wilaya Wanusurika Sakata la Vyeti FEKI
Kairuki amebainisha hayo leo katika ukumbi wa Chimwaga uliopo ndani ya Chuo Kikuu cha Dodoma, wakati anatoa taarifa ya uwasilishaji wa uhakiki wa vyeti feki kwa Watumishi wa Umma lilioendeshwa na Serikali kuanzia mwezi Oktoba mwaka 2016.
"Zoezi hili la uhakiki wa vyeti feki halikuwahusisha viongozi wa kisiasa kama Wabunge, Mawaziri, Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya, kwa sababu kwa mamlaka za uteuzi wao wanahitajika kujua kusoma na kuandika tu...Watumishi 9,932 wamebainika kuwa na vyeti vya kughushi sawa na asilimia 2.4 . Wenye vyeti vya utata ni 1,538 vilikuwa vikitumiwa na jumla ya watu 3,076, wenye vyeti halali pekee ni asilimia 94...Hatua hazitachukuliwa kwa wenye vyeti feki tu, bali hata kwa wanaohusika kutengeneza vyeti hivyo". Alisema Kairuki
Aidha Mhe. Kairuki amewataka wale wote wanajijua wanatumia vyeti vya kughushi waache mara moja kwa kuwa ni kosa la jinai huku akisisitiza kuwa adhabu yake ni kufungwa jela miaka saba.
Pamoja na hayo, Kairuki amepongeza serikali inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli kwa kuamua kushughulika na zoezi hilo na kulimaliza kwa awamu moja tofauti na nchi nyingine zilichukua awamu tatu huku akitolea mfano wa kwa kuzitaja nchi hizo kwamba ni South Africa na Nigeria.
Kwa upande mwingine, Rais Dkt. Magufuli amewaagiza Waziri Kairuki na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuwaondoa watumishi wote waliobainika kuwa wanatumia vyeti vya kughushi 'hewa' huku akisisitiza kwamba yeye hawezi kuwasemehe watu walioghushi kwani wataondoka mara moja.
CUF Lazima Kuchafuke: Wabunge Upande wa Maalim Wamepanga Kufanya Usafi Ofisi Kuu, Kambi ya Lipuma Imejipanga Kuwazuia
Wapinzani
wawili katika mgogoro wa uongozi wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad na
Profesa Ibrahim Lipumba sasa wamefikia pabaya baada ya kuamua kupambana
kuichukua ofisi ya makao makuu iliyopo Buguruni.
Kwa
sasa ofisi hiyo inatumiwa na Profesa Lipumba, ambaye uamuzi wake wa
kurejea madarakani mwaka mmoja baada ya kujiuzulu uenyekiti na nyadhifa
nyingine zote, unapingwa na kundi lililopanga kuzichukua ofisi hizo
Jumapili.
Jana,
kundi linalompinga Profesa Lipumba lilitangaza kuwa litakwenda ofisi
hizo Jumapili kwa ajili ya kusafisha “kila kitu ambacho hakitakiwi
kiwepo”, lakini mwenyekiti huyo amesema ameshajiandaa kukabiliana nao na
ameripoti suala hilo polisi.
Profesa
Lipumba alisema hayo jana, ikiwa ni siku moja tangu Jukwaa la Wahariri
Tanzania (TEF) limtake ajitokeze kuzungumzia kitendo cha walinzi wa CUF
kuwashambulia waandishi wa habari waliokuwa kwenye mkutano ulioandaliwa
na viongozi wa chama hicho Kinondoni.
Profesa
Lipumba alikuwa akiwajibu wabunge wa CUF wanaomuunga mkono Maalim Seif
waliowaambia wanahabari katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma jana kuwa
wamepanga kwenda ofisi za Buguruni Jumapili ijayo na wataungana na
wanachama wengine kufanya usafi.
“Tulianza
kufanya usafi soko la Buguruni, tukamalizia katika ofisi yetu. Kwa hiyo
katika hali nzuri, hatuhitaji wabunge wasumbuke kufanya usafi siku
hiyo,” alisema Profesa Lipumba
Profesa
Lipumba alisema watu hao hawana nia ya dhati ya kufanya usafi, bali
wamepanga kufanya vurugu katika ofisi hizo kwa kushirikiana na watu wa
chama kingine cha upinzani.
“Wanataka
kuleta vurugu ili CUF ionekane na taswira mbaya kwa Watanzania. Naomba
wanachama waepuke mtego huu, namshauri (Mbunge wa Temeke, Abdallah)
Mtolea akafanye usafi huo Temeke mbona kuna masoko mengi tu machafu?” alisema.
Awali mjini Dodoma, wabunge wanaomuunga Maalim Seif walisema watakwenda na vifaa vya usafikuondoa kila uchafu watakaoukuta
“Wanachama
wa Chama cha Wananchi (CUF) ambao hawamkubali Profesa Ibrahim Lipumba
kuwa mwenyekiti, wameamua kwenda kufanya usafi kwenye ofisi zao za
Buguruni, ofisi kuu ya CUF Buguruni,” alisema Mtolea akiwa ameambatana na wabunge wenzake katika mkutano na waandishi uliofanyika chumba cha habari cha Bunge.
“Na
hatua hii imekuja baada ya kuona ofisi ile inatumika vibaya. Imekuwa
ndio kijiwe cha wahuni kupanga matukio ya kihalifu. Kwenda kuvamia
mikutano, kwenda kuwavamia watu na kadhalika. Sasa sisi kama wanachama
tumeona hatuwezi kuiacha hali hiyo iendelee.”
Aliwataka wanachama kutoka maeneo ya Dar es Salaam, Pwani na mikoa mingine wafike kufanya usafi huo.
Alipoulizwa
aina ya uchafu wanaoenda kuuondoa, Mtolea alijibu “ni kitu chochote
ambacho hakiko mahali pake” na kwamba hata Profesa Lipumba hayuko mahali
pake.
“Tangu
Msajili amtambue Profesa Lipumba kuwa mwenyekiti, hatujawahi kwenda
katika ofisi yetu ya Buguruni, matokeo yake ofisi hiyo imekuwa na uchafu
mwingi na kuwa pango la wahuni,” alisema Mtolea.
Alipoulizwa uwezekano wa kutokea vurugu, Mtolea alisema hawajiandai kufanya fujo, bali kufanya usafi.
Kuhusu
kesi iliyopo mahakamani kuhusu mgogoro huo, alisema ile inapinga
msajili kumtambua Lipumba na haizuii kusafisha ofisi yao.
Alisema hawaendi kuteka ofisi hizo, bali wanakwenda kwenye ofisi zao hivyo hawahitaji kuomba ruhusa kwa mtu yeyote.
“Ofisi ni chafu, sisi tunataka tukaisafishe kwa sababu imekuwa sehemu ya kupanga mipango mibaya kwa mustakabali wa chama,” alisema.
Akiweka msisitizo wa jibu hilo, Mbunge wa Chambani, Yusuf Salim Hussein alisema hakuna silaha ya moto inayoshinda nguvu ya umma.
Awali,
wabunge hao walitoa tamko la kuunga mkono tamko la TEF kuhusu kulaani
kitendo cha wafuasi wa Profesa Lipumba kuwashambulia waandishi wa
habari.
Mnadhimu
wa chama hicho na Mbunge wa Malindi, Ally Salehe alisema TEF imetoa
tamko zito la kutaka waandishi wa habari kufanya kazi kwa usalama na
uhuru.
“Na isiwe TEF tu, tunataka watu wote waliokerwa na tukio hilo watoe tamko la kulaani,” alisema.
Kuhusu tamko la TEF, Profesa Lipumba alisema atatoa tamko kuhusu suala hilo ifikapo leo.
“Mimi
ni muumini wa demokrasia. Hapa ninavyoongea na wewe nipo katika hatua
ya mwisho ya kumalizia kuandika barua kuelekea TEF ambayo itafika kati
ya leo (jana) jioni au kesho,” alisema.
Hata hivyo, alisema mkurugenzi wa habari, uenezi na mawasiliano kwa umma, Abdul Kambaya alitoa tamko kuhusu tukio hilo.
CCM: Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Atiwa Mbaroni
Jeshi la Polisi mkoani Iringa linamshikilia mwenyekiti wa zamani wa
Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Iringa, Jesca Msambatavangu, kwa
tuhuma za kumshambulia mwanamke mmoja na kumsababishia maumivu makali
mwilini.
Msambatavangu, ambaye alikuwa miongoni mwa wanaCCM
waliofukuzwa uanachama katika Mkutano Mkuu Maalum wa chama hicho
uliofanyika mwezi Machi, alikamatwa jana mchana
Kamanda
wa Polisi mkoani Iringa, Julius Mjengi, alisema kuwa
kiongozi mstaafu anatuhumiwa kutenda kosa hilo wiki iliyopita.
Akifafanua,
Kamanda Mjengi alibainisha kuwa kiongozi huyo alitenda kosa hilo akiwa
na wenzake ambao asingeweza kuweka majina yao hadharani kwani
wanaendelea kuwatafuta.
"Ni kweli tunamshikilia Jesca
Msambatavangu, tumemkamata leo(jana) saa nane mchana na tunaendelea na
uchunguzi dhidi yake," alisema Mjengi na kuongeza:
"Jesca pamoja
na wenzake wanatuhumiwa kumshambulia mwanamke mmoja mkazi wa Kibwabwa,
walimshambulia na kisha kumchoma sindano ambayo mwanamke huyo hajui ni
ya kitu gani," alisema Mjengi.
Alipohojiwa zaidi, Mjengi alikataa
kuweka wazi jina la mwanamke na idadi ya watuhumiwa wengine kwa maelezo
kuwa kufanya hivyo kunaweza kuharibu upelelezi unaoendelea.
MIGODI INAYOMILIKIWA NA KAMPUNI YA ACACIA YAWA KIVUTIO KATIKA MAONESHO YA WIKI YA USALAMA NA AFYA MAHALA PA KAZI
Maonesho ya Wiki ya Usalama na Afya mahala pa kazi yanayofanyika Moshi mkoani Kilimanjaro.
Maonesho haya yanayohusisha kampuni na Taasisi mbalimbali nchini yanaratibiwa na Wakala wa Usalama na Afya mahala pa Kazi (OSHA).
Baadhi ya Wafanyakazi wa Mgodi wa
Dhahabu wa Bulyanhulu unaomilikiwa na Kampuni ya ACACIA,wakiweka sawa
moja ya picha inayoonesha eneo ambalo shughuli za uchimbaji unafanyika.
Afisa Uhakiki na Usalama katika Mgodi wa Dhahabu wa
Bulyanhulu unaomilikiwa na kampuni ya ACACIA,Amina Mohamed akitoa
maelezo kwa wananchi waliotembelea banda hilo.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Mgodi wa Dhahabu wa
Bulyanhulu unaomilikiwa na Kampuni ya ACACIA,wakitoa maelezo kwa
wananchi waliotembelea banda hilo katika maeonesho ya wiki ya usalama
mahala pa kazi ndani ya viwanja vya Chuo Kikuu cha Ushirika mjini Moshi.
Afisa Afya katika Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu
,Tumaini Sylivanus akitoa maelezo ya namna wanavyotoa huduma ya Afya kwa
wafanyakazi wa Mgodi huo pindi wapatapo matatizo.
Mmoja wa Wakazi wa Kilimanjaro akipewa maelekezo ya
namna ya kutumia kifaa maalumu kinachotumika katika zoezi la uzimaji wa
moto pindi yatokeapo majanga ya Moto.Nyuma yake ni mmoja wa wafanyakazi
wa Mgodi wa Bulyanhulu unaomilikiwa na kampuni ya ACACIA.
Afisa Viwango wa Mgodi wa Dhahabu wa
Bulyanhulu,Setieli Kimaro akitoa ufafanuzi kwa wananchi waliotembelea
banda la modi huo unaomilikiwa na kampuni ya ACACIA.
Afisa Usalama katika Mgodi wa Buzwagi unaomilikiwa na
Kampuni ya ACACIA,Deogratius Nyantabano akitoa maelezo kwa wanafunzi
waliotembelea banda la mgodi huo katika maonesho ya wiki ya usalama na
afya mahala pa kazi yanyofanyika katika uwanja wa Chuo Kikuu cha
Ushirika Moshi ,Kilimanjaro.
Afisa Usalama katika Mgodi wa Buzwagi unaomilikiwa na
Kampuni ya ACACIA,Mustapher Mlewa akieleza jambo kwa baadhi ya wananchi
waliotembelea Banda hilo.
Daktari kutoka Mgodi wa Buzwagi unaomilikiwa na
Kampuni ya ACACIA,Dkt Ludovick Silima akitoa maelezo juu ya usalama kwa
mmoja wa wananchi waliofika katika banda la mgodi huo wakati wa maonesho
ya wiki ya usalama na afya mahala pa kazi yanayoendelea katika viwanja
vya Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi.
Afisa Mazingira katika Mgodi wa north Mara ,Sara
Cyprian akionesha picha na maelezo kwa baadhi ya wananchi waliotembelea
banda la Mgodi huo katika maonesho ya wiki ya usalama na afya mahala pa
kazi.
Afisa Usalama katika mgodi wa Dhahabu wa North Mara
unaomilikiwa na kampuni ya ACACIA,Samweli Nansika (aliyenyoosha kidole)
akitoa maelezo kwa baadhi ya wananchi waliotembelea banda la mgodi huo.
Mkuu wa Idara ya Usalama na uokoaji katika Mgodi wa
Dhahabu wa North Mara ,Emanuel Erasto(katikati) akitoa maelezo namna
amavyo wanaweza kumuokoa mtu aliyepata athari iliytokana na kemikali.
Eneo maalumu la kumuogesha mtu aliyepata athari ya kemikali.
Afisa usalama akita huduma ya kumsafisha mtu
aliyepata athali ya kemikali akiwa nje ya bafu hilo la kumuogeshea ili
na yeye asipate madhara.
Wafanyakazi wa Mgodi wa Buzwagi wakionesha namna ambavyo wanaweza msaidia mtu aliyepatwa na janga la Moto.
Kifaa Maalumu kinachotumika katika kubeba mwili wa mtu aliyepata madhara akiwa katika shimo wakati wa uchimbaji wa Dhahabu.
Mmoja wa wafanyakazi wa Mgodi wa Bulyanhulu akitoa
maelezo kwa wananchi walitembelea banda hilo namna ambavyo wanaweza
kunyanyua Gari pamoja na Mawe yaliyomuangukia mtu wakati akitekeleza
majukumu yake kwa kutumia kifaa maalumu kinachojazwa upepo (Air Bag).
Mkuu wa Idara ya Usalama na Uokoaji katika Mgodi wa
North Mara ,Emanuel Erasto akitoa maelezo namna wanavyoweza kumukoa mtu
aliyepatwa madhara akiwa chini ya mgodi .
Dkt Ludovick Silima akitoa ufafanuzi kwa wananchi waliotembelea banda la Mgodi wa Buzwagi.
Afisa Mahusiano katika Mgodi wa Bulyanhulu akitoa
maelezo ya namna Mgodi huo unavyo tekeleza majukumu yake ukitoa
kipaumbele katika masuala ya Usalama na Afya kwa watumishi wake.
Afisa Uhusiano wa Mgodi wa Buzwagi ,Magesa Magesa
akitoa maelezo namna mgodi huo ulivyoshiriki katika shughuli za
maendeleo ikiwemo ujengaji wa vyumba vya madarasa,zahanati,maji pamoja
na suala la kuhamasisha michezo katika maeneo yanayozunguka mgodi huo.
Na Dixon Buagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
Waziri Masauni: Waliolipua Bomu Nyumba ya Kamishna wa Polisi Zanzibar ni Viongozi wa CUF
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni
amesema viongozi waandamizi wa chama cha wananchi (CUF) ndiyo walihusika
na tukio la kulipua bomu katika nyumba ya Kamishna wa Jeshi la Polisi
Zanzibar baada ya kufanyika uchaguzi mkuu
Mhe. Masauni alieleza hayo Bungeni Jijini Dodoma jana pindi
alipokuwa akijibu swali la nyongeza kutoka kwa Mbunge wa Gandu kupitia
tiketi ya (CUF) visiwani Pemba, Mhe. Othuman Omary Hajji alipotaka kujua
kwanini mpaka leo hajizachukuliwa hatua stahiki kwa wafuasi wa CCM
waliochoma nyumba za wanachama wa CUF huko visiwani Tumbatu, huku akidai
serikali iliyopo madarakani siyo halali ni haramu kwa kuwa Jeshi la
Polisi lilichangia kumuweka madarakani Dkt. Ali Mohamed Shein.
"Ni kweli baada ya uchaguzi mkuu baadhi ya vyama vya
upinzani ikiwemo chake, viongozi walijitokeza kuhamasisha wananchi
kufanya mambo yanayokiuka sheria za nchi yetu.
"Kuna matukio mbalimbali yalijitokeza ikiwemo kuchomwa
moto nyumba, kuchoma mashamba, kurusha mabomu ikiwemo nyumba ya Kamishna
wa Jeshi la Polisi wa Zanzibar ambayo kwa uchunguzi uliofanyika mpaka
sasa, watu waliokamatwa kwa kuhusika urushaji bomu katika nyumba ya
Kamishna ni viongozi waandamizi wa Chama cha Wananchi (CUF)". Alisema Masauni
Pamoja na hayo, Masauni alisema Jeshi la Polisi
limeshakamilisha uchunguzi wake na jalada la mashtaka lipo kwa DPP muda
wowote kuanzia sasa litapandishwa Mahakamani ili sheria ichukuliwe.Ray Kigosi afunguka Mambo Mazito kuhusu marehemu Kanumba Kuhusishwa na Uchawi na Freemason
Msanii wa filamu nchini Ray Kigosi amefunguka na kusema
kuwa baadhi wa Watanzania ni wanafiki na wamekuwa wakikatisha tamaa watu
katika mambo yao kutokana na unafiki wao.
Ray Kigosi amesema hayo kupitia ukurasa wake wa Instgram na
kusema kutokana na unafiki huo wa baadhi ya watu ulimfanya mpaka
marehemu Kanumba kuvunjwa moyo katika kazi yake.
==>Ray Kigosi ameandika;
1. Kanumba alipoanza kuona mwanga wa kufanikiwa bila kujali juhudi zake kuna watu walimuita Freemanson, Mara anatumia nguvu za Giza. that is to say films zake hazikuwa nzuri but ziliuza sababu ya nguvu za Freemanson na nguvu za giza!!
1. Kanumba alipoanza kuona mwanga wa kufanikiwa bila kujali juhudi zake kuna watu walimuita Freemanson, Mara anatumia nguvu za Giza. that is to say films zake hazikuwa nzuri but ziliuza sababu ya nguvu za Freemanson na nguvu za giza!!
2. Kanumba alipoenda Big Brother alipondwa Sana na kuitwa
bogus kwa Madai hajui kiingereza, Ni watanzania Hawa Hawa walibebea
bango hili huku baadhi ya waandishi uchwara wakieneza ujinga huu bila
kujali juhudi zake. But Leo wanamsifia hakuna Kama Kanumba!
3. Kuna wakati Kanumba alionekana wazi kuvunjwa moyo na
kukatishwa tamaa kwa kuonekana juhudi zake si kitu. But Alisema maneno
machache Kuwa mtanikumbuka kama si Leo basi Ni Kesho.
And alichosema kimetimia, wale wale waliokuwa wakisema Ni Freemanson bila hata kujali juhudi zake kwenye game Leo ndio kwa unafiki wanasema hakuna Kama Kanumba !….. HAO NDIO BINADAMU NA TABIA ZAO
Je Kanumba kaondoka na Bongo Movie yake ya Freemanson ? Kama wengine mnavyodhani industry Ni Mtu sio system !
4. Diamond Platnumz nae baada ya kuona Njia ya mafanikio
kuna watanzania, wasanii wenzake na hata baadhi ya wanahabari wanasema
Ni Freemanson, wengine wanaonyesha chuki ya wazi kwake. Wanasema Hana
muziki mzuri, Mara Ni Kiki tu ambazo hata Kanumba alikuwa akiripotiwa
magazetini na kina Wema.
Hawaoni juhudi na thamani ya Diamond sasa ! Hatuombi baya
limpate Diamond ili kudhibitisha tabia na unafiki wa binadamu. But HAO
NDIO BINADAMU siku zote hawana Jema unafiki ni sehemu ya Maisha.
5. kila siku Ni kuzua hii na kile, Mara ooh Diamond Ni
mchawi, kasema mleteni huyo mganga wangu mkashindwa kumleta, akajitokeza
mganga fake sijui na Madai juu Kuwa Diamond atashuka kimuziki kwa
sababu ananipuuza niliyempa nyota, Diamond akasema sawa namtegemea
Mungu. Miaka 4 sasa tangu yaliyoitwa ya mganga Diamond hashuki ndio
anazidi kupaa. HAO NDIO BINADAMU kusema lolote Ni haki Yao.
Kazi za Kanumba sasa zinapewa thamani na ubora uliovuka
mipaka na viwango ambao hakupewa kipindi yupo hai ! HAO NDIO BINADAMU na
tabia zao. Ni tabia tu ya baadhi ya watu kubebea mabango mabaya ya Mtu
au uzushi na kuacha mazuri yake then baadaye wakishikwa Uchawi wanageuza
walichoamini Ni nyeusi kiwe nye.
MWANARIADHA SIMBU APOKELEWA BUNGENI
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe.
Dkt. Harrison G. Mwakyembe (Mb), leo tarehe 27 Aprili, 2017 amempokea
mwanariadha na mshindi wa tuzo ya dhahabu kwenye Mumbai Marathon Bw.
Alphonce Simbu na kumtambulisha kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dodoma. Bw. Simbu aliongozana na Viongozi Waandamizi wa Jeshi
la Kujenga Taifa ameweza pia kukutana na Mhe. Kassim M. Majaliwa,
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Wabunge na
Viongozi mbalimbali wa Serikali.
Alhamisi, 27 Aprili 2017
Kenya imepiga marufuku gesi ya kupikia ya Tanzania kuingizwa nchini humo.....Zitto Kabwe Aitaka Serikali Ichukue Hatua
Wizara
ya Nishati ya Kenya imepiga marufuku gesi ya kupikia kutoka Tanzania
kuingia nchini humo. Tamko la Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati ya Kenya
linasema ‘ ndani ya siku 7 kuanzia juzi tarehe 24 Aprili 2017, itakuwa
ni marufuku Kwa Kenya kuagiza Gesi ya kupikia kutoka Tanzania ‘.
Uamuzi
huu wa Kenya ni kinyume na misingi ya Jumuiya ya Afrika Mashariki
ambapo Tanzania na Kenya ni wanachama. Kwa mujibu wa Itifaki ya Soko la
Pamoja, bidhaa za nchi zetu zinaruhusiwa kusambaa ndani ya jumuiya bila
vikwazo.
Gesi
ya kupikia kuingia Kenya hutokea Tanzania Kwa sababu Tanzania ni nchi
pekee katika ukanda huu ambayo imewekeza mitambo ya kupokea Gesi na
kuiweka kwenye mitungi. Bandari ya Dar Es salaam na mfumo mzuri zaidi wa
kupokea gesi kuliko Bandari ya Mombasa na hivyo kuifanya gesi inayotoka
Tanzania kuwa na gharama nafuu nchini Kenya kuliko gesi inayoagizwa
kupitia bandari ya mombasa.
Uamuzi
wa kuzuia Gesi kutoka Tanzania ni uamuzi wenye kulenga kuilinda bandari
ya Mombasa Kwa kuvunja mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Kwa
kutaka kuifanya Tanzania iendelee kuwa muuzaji wa malighafi kwenda Kenya
badala ya bidhaa zilizokamili Kama gesi ya kupikia.
Uamuzi
huu wa Serikali ya Kenya una lengo la kuathiri urari wa biashara kati
ya Tanzania na Kenya ambapo Kwa miaka ya hivi karibuni Tanzania imekuwa
ikiuza bidhaa nyingi zaidi huko Kenya kuliko inazoagiza kutoka nchi
hiyo.
Ninamsihi
Waziri wa Biashara na Viwanda wa Tanzania afuatilie suala hili na
kuzungumza na mwenzake wa Kenya ili waondoe vikwazo Hivi vya biashara
ambavyo havina maana yeyote na vinazuia raia wa kenya kupata bidhaa
nafuu kutoka Tanzania.
Viwanda
vingi vya Kenya hutegemea malighafi kutoka Tanzania, kuzuia gesi ya
kupikia na kuendelea kuagiza malighafi za kuendesha viwanda vyao ni sera
ya Kenya kuifanya Tanzania kuwa chanzo cha malighafi tu na sio chanzo
cha bidhaa zilizoongezwa thamani.
Serikali
ya Tanzania isikubali hili na ianze mazungumzo mara moja na Serikali ya
Kenya ili Watanzania wanaouza gesi ya kupikia huko Kenya waendelee
kuuza na kutumia Bandari ya Dar Es Salaam.
Kama
Serikali ya Kenya ikiendelea na msimamo wake basi Tanzania ichukue
msimamo kama huo Kwa bidhaa za Kenya Kama maziwa ambayo yamejaa kwenye
soko letu.
Zitto Kabwe, Mb
Kigoma mjini
26/4/2017
Rais Magufuli: Olewak Atakayethubutu Kuuvunja Muungano
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli,
leo tarehe 26 April 2017, ameongoza maelfu ya Watanzania katika sherehe
za miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika katika
Uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma.
Akizungumza
mara baada ya kukagua gwaride la vikosi vya ulinzi na Usalama
lililoandaliwa kwa heshma yake, Rais Magufuli amewahakikishia watanzania
kuwa yeye na Rais wa Zanzibara Dkt. Ali Mohamed Shein wataendelea
kuulinda Muungano kwa nguvu zao zote na kwamba atakayejaribu kuuvunja
atavunjika yeye.
''Muungano
ndio silaha yetu. Ni nguvu yetu. Mimi na mwenzangu Dkt. Shein
tutaulinda Muungano kwa nguvu zote. Yeyote atakayejaribu kuuvunja
atavunjika yeye'' amesema Rais Magufuli.
Aidha
Dkt. Magufuli amewataka watanzania kuendelea kudumisha amani iliyopo
nchini kwani amani ndio chachu ya maendeleo yanayopatikana nchini.
Rais
Magufuli amesema Tanzania imeweza kufikisha miaka 53 ya Muungano wa
Tanganyika na Zanzibar kwa sababu ya amani iliyopo nchini iliyowezesha
kupatikana mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kuunganisha mataifa yetu
mawili na kuuunda taifa moja lenye nguvu.
Aidha
amesema Muungano wa Tanganyika na Zanzibar umewezesha kupatikana
mafanikio makubwa katika nyanja za kiuchumi, kisiasa na kijamii.
Mhe.
Rais ametaja mafanikio mengine yaliyopatikana kutokana na Muungano ni
kukua kwa uchumi na kukabiliana na matatizo ya umasikini na ukosefu wa
ajira,kuimarisha miundombinu ya usafiri wa anga, majini,reli na nchi
kavu.
Aidha
Muungano umeimarisha na kuboresha upatikanaji wa huduma za jamii ikiwa
ni pamoja na kuongezeka kwa idadi ya shule na hospitali pamoja na kukua
kwa demokrasia nchini.
Kwa
mara ya kwanaza katika historia ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
Maadhimisho ya Sherehe za Muungano zinafanyika mkoani Dodoma makao makuu
ya Serikali ikiwa ni ishara tosha kuwa Serikali ya awamu ya tano
inayoongozwa na chama cha Mapinduzi imedhamiria kwa dhati kuhakikisha
makao makuuu ya Serikali yanakuwa Dodoma.
''Niwahahakikishie
wana Dodoma na Watanzania kwa ujumla kwamba Serikali sasa tumefika
Dodoma na hatutarudi tena, na kama tulivyoahidi mwaka 2020 Serikali
yote itakuwa imehamia hapa'' amesema Rais magufuli.
Sherehe
za miaka 53 ya Muungano zimehudhuriwa na viongozi mbalimbali ikiwa ni
pamoja na wajane wa viongozi waasisi wa Muungano mke wa hayati Mwalimu
Julius Nyere Mama Maria Nyerere na hayati Abeid Aman Karume, Mama Shadya
Karume,Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim
Majaliwa, na viongozi wa chama na serikali.
Kauli
mbiu ya Sherehe za Muungano mwaka huu ni ''Miaka 53 ya
muungano,Tuuulinde na kuuimarisha, Tupige vita Dawa za Kulevya na
Kufanya Kazi kwa Bidii''
Jaffar Haniu
Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dodoma
26 Aprili, 2017
Marekani yaanza kujenga mtambo kuzuia makombora ya Korea Kaskazini
Korea Kusini imesema wanajeshi wa Marekani wameanza kujenga mtambo wa
kisasa wa kuzuia makombora katika eneo moja kusini mwa nchi hiyo.
Mtambo huo wa kujilinda dhidi ya makombora, ambao hufahamika kitaalamu
kama THAAD, kwa Kiingereza Terminal High Altitude Area Defense, kutokana
na wasiwasi wa tishio kutoka kwa Korea Kaskazini ambayo imeendelea
kufanyia majaribio makombora.
Wizara ya ulinzi ya Korea Kusini imesema mtambo huo utakamilishwa an utakuwa tayari kutumika katika kipindi cha mwaka mmoja.
Kumekuwepo na taarifa za kutokea kwa makabiliano kati ya wenyeji na
polisi eneo panapojengwa mtambo huo, ambalo awali lilikuwa uwanja wa
mchezo wa gofu.
Mtambo huo unajengwa katika wilaya ya Seongju
China imekuwa ikipinga kuwekwa kwa mtambo huo.
Rais wa Marekani Donald Trump ameashiria kwamba Marekani iko tayari
kuchukua hatua kivyake bila kuishirikisha China kukabiliana na tishio la
nyuklia kutoka kwa Korea Kaskazini.
THAAD ni nini?
- Ni teknolojia ya kujilinda ya kutungua makombora ya masafa mafupi na wastani ambayo huyaharibu yanapokaribia kulipuka.
- Hugonga kombora la kuliharibu
- Ina uwezo wa kufika umbali wa kilomita 200 na inaweza kurushwa juu hadi kilomita 150 angani
- Marekani imewahi kuweka mitambo kama hiyo Guam na Hawaii kujilinda dhidi ya uwezekano wa mashambulizi kutoka kwa Korea Kaskazini.
Chanzo: BBC
Baada
ya Mwimbaji Ray C kuachia wimbo wake wa Unanimaliza, Msanii wa
BongoFleva, Diamond Platnumz kupitia account yake ya Instagram ameandika
ujumbe huu
"Salaam dada angu @rayctanzania , siku ya leo nilitamani nikwambie maneno haya: Spirit ama juhudi unayoionyesha sasa inatia faraja sana, naamini sio kwa wapenda muziki wa Tanzania tu bali hata kwa watu mbalimbali….
"Nafarijika
kuona wimbo wako wa #Unanimaliza watu mbalimbali wameupokea vizuri, na
nisiwe mnafiki hata mie ni miongoni mwa watu wanaoupenda wimbo huu
wako mpya…. Ombi langu kwako usikubali kurudi nyuma tena, ijapokuwa
sanaa zetu zina changamoto nyingi ila amini ni mitihani tu ya Mwenyez
Mungu, ila ukiwa mvumilivu na kumuomba Muumba, itapita….
"niwaombe
pia Vyombo vya Habari vyetu pendwa tuzidi kumsapoti dada etu, kwani
naami kwa sapoti yenu, sapoti ya wadau mbalimbali na kuongeza juhudi
kwake kutamfanya awe mfano bora, na kuamsha vijana wengi sana mitaani
kwetu ambao pengine walijikatia tamaa kwa mambo mbalimbali….InshaAllah
Mwenyez Mungu akusmamaie katika kazi zako na Maisha ya kila siku"
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)