Powered by: Elbahsan Web & Blog Designer
Do want your Network!!! Website or Blog-Spot, Try Us: Elbahsan Web & Blog Designer Contact Us Now... Calll; +255743550360 | +255788680558 Email; murtadhaalbahsan@gmail.com

Zawamba Photo Production

Jumanne, 30 Mei 2017

Mamlaka ya hali ya hewa yatoa tahadhari kwa wakazi wa ukanda wa pwani

Mamlaka ya hali ya hewa imetoa tahadhari  kubwa kwa wakazi wa ukanda wa pwani kuwa kutakuwepo na upepo mkali na mawimbi makubwa katika maeneo ya bahari ya Hindi.

Aidha, katika Maeneo yanayotarajiwa kukumbwa na hali hiyo ni pamoja na mikoa ya Mtwara, Lindi, Pwani, Dar es Salaam, Tanga pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.

Katika taarifa iliyotolewa na Mamlaka hiyo, imesema kuwa kunatarjiwa kuwepo na upepo mkali wa kasi ya kilomita 40 kwa saa na mawimbi yanayozidi mita 2 baharini hivyo watumiaji wote wa bahari wametakiwa kuchukua tahadhari kubwa.

Hata hivyo, hali hiyo inasababishwa na msukumo wa upepo wa kusi unaotokana na kuimarika kwa mgandamizo mkubwa wa hewa katika ukanda pwani hivyo kusababisha hali hiyo kutkea.

Walemavu walioungana wampata kijana wa kuwaoa

Kwa yeyote aliyewahi kukutana nao, mapacha wawili ambao ni walemavu walioungana matumbo, Maria na Konsolata hatabisha kwamba pamoja na hali yao, watoto hao ni wacheshi, wakarimu na wanaoweza kukufanya utabasamu hata kama moyoni mwako, ulikuwa na huzuni
Wiki hii walifanyiwa mahojiano na Gazeti la Mwananchi na kufunguka mengi kuhusu maisha yao pamoja na ishu yao ya kufikiria kuolewa.

    Si rahisi kufikiria maisha ya ndoa ya Maria na Consolata kwa jinsi walivyo, lakini pacha hawa walioungana wako wazi kuhusu matamanio yao ya maisha ya ndoa.

    Katika mazungumzo yao na gazeti hili, Maria na Consolata waliweka bayana mipango yao ya ndoa mara watakapomaliza elimu ya chuo kikuu.

    Ingawa ni kitu cha kushangaza, Maria na Consolata hawatakuwa mapacha wa kwanza katika maisha ya ndoa. Chang na Eng Bunker ni pacha wanaume waliozaliwa mwaka 1811 nchini Thailand ambako zamani kuliitwa Siame.

 Tofauti na mapenzi ya akina Maria na Consolata, pacha hao kila mmoja alioa mke wake na kufanikiwa kupata watoto.
Kama ilivyokuwa kwa pacha hao, Maria na Consolata wanatamani kuwa wanandoa na ndoto zao ni kuolewa na mwanaume mcha Mungu na atakayewajali.

    “Ndoa ni sakramenti takatifu, tukishamaliza masomo yetu ya chuo kikuu tunatamani kuja kuwa wanandoa,” anasema Maria.

    Kwa namna walivyo, si rahisi kwao kuolewa na wanaume tofauti isipokuwa mume mmoja na wanalijua hilo.

    Haya ndio yalikuwa mahojiano baina yangu na wao kufuatia ndoto hiyo.

    Mwandishi: Baada ya masomo, nini ndoto zenu?

    Maria: Ndoto zetu ni kuwa wanandoa. Zamani tulikuwa tunapenda tofauti, lakini kwa sasa tumempenda mtu mmoja.

    Tumegundua tuna hisia moja.

    Mwandishi: Tayari kuna mtu mmempenda nini?

    Maria na Consolata kwa pamoja: Ndio tumempenda mtu mmoja.

    Mwandishi: Nani alimwambia mwenzake kwanza kuhusu hisia za kupenda?

    Consolata: Sisi ndio tuliomwambia kwamba tunampenda, naye alitusikiliza.

    Mwandishi: Aliwajibu nini?

    Maria: Yupo kwenye tafakari, hawezi kusema akurupuke na kuingia bila tafakari. Lazima tumpe muda wa kutafakari.
    Mwandishi: Ni mwanaume wa aina gani mnayempenda?

    Consolata; Tunapenda kuolewa na mwanaume wa kawaida, mwenye tabia njema na mcha Mungu asiwe tajiri. Ikiwa tutamaliza masomo yetu, huyu tuliyempenda anafaa kuwa mume wetu. Kihalisia tunatamani mwanaume mcha Mungu, mwenye upendo na ambaye atathamini utu wetu.

    Mwandishi: Kwa nini hampendi kuolewa na tajiri?

    Consolata: Ni kwa sababu matajiri wengi huwa wanathamini pesa zao sio utu. Samahani hapa sio matajiri wote, ila wengi wao kwa hiyo sisi tunataka mtu anayeweza kuthamini utu.

    Mwananchi: Ndoa ni mume na mke mmoja kwa Wakristo. Mmewahi kutafakari hilo?

    Consolata; Ndio, Biblia inasema kwamba Mungu aliweka agano kati ya mume na mke mmoja. Sasa kwa kuwa sisi tumeungana wawili na tuna hisia moja, hatuwezi kuolewa na wanaume tofauti. Tutaolewa na mume mmoja.

    Tunatamani sana kumtumikia Mungu kupitia sakramenti ya ndoa. Mungu akitujalia tumalize masomo yetu basi tunataka kuolewa ili tumtumikie Mungu katika huo wito vizuri.

    Pacha hao waliweka bayana jina la kijana waliyempenda, ingawa kwa sababu za kimaadili tunalihifadhi. Hata hivyo, baba mdogo wa kijana huyo alikuwa tayari kuzungumza na gazeti hili.

    Baba huyo mdogo alisema ana taarifa za kijana wao kupendwa na pacha hao.

    “Unajua nilishangaa kuona watu wananiita baba mkwe wa akina Maria na Consolata. Baadaye ndio nikajua kuwa kuna mahusiano baina yao (kijana na mapacha hao), japo wote wanaendelea na masomo. Kupenda ni moyo na kama ikitokea wakafikia ndoto hizo huko baadaye, basi itakuwa hivyo,” anasema.

    Mwalimu mkuu wa Shule ya Maria Consolata, Jefred Kipingi anasema hisia za kuolewa kwa mabinti hao ni jambo la kawaida na kwamba, wanapenda kuishi maisha ya kawaida kama walivyo watu wengine.

    “Uzuri wake ndoto yao ni kuwa walimu na wanasema wataolewa wakishamaliza masomo yao. Jambo hilo ni jema na hapo Mungu ndipo atadhihirisha utukufu wake zaidi,” anasisitiza.

    Ingetegemewa kwamba katika dunia ya utandawazi, taarifa za kuzaliwa kwa pacha walioungana zingetapakaa kila mahali zikipamba magazeti, redio, luninga na hata mitandao ya kijamii.

    Lakini haikuwa hivyo kwa Maria na Consolata. Hakuna chombo chochote kilichopata taarifa ya kuzaliwa kwa pacha hao wa kipekee.

    Ulemavu wao ulisababisha wafichwe hadi walipofikisha umri wa kuandikishwa elimu ya msingi katika Shule ya Ikonda na kutafutiwa mlezi wa kuwaangalia, baada ya wazazi wao kufariki dunia wakiwa wadogo.

    Habari zao zilianza kufahamika baada ya kuandikishwa darasa la kwanza na kutafutiwa mlezi aliyewalea hadi wakati walipofaulu vizuri mitihani yao ya darasa la saba mwaka 2010.

    Mlezi wao, Bestina Mbilinyi alikuwa alifanya hivyo chini ya wamisionari lakini, alikuwa akiishi nao nyumbani kwake Ikonda.

    “Niliombwa niishi na watoto hawa kwa sababu kutoka kwangu hadi shuleni sio mbali, nilijengwa choo kinachokidhi maumbile yao na niliishi nao hadi wanamaliza darasa la saba,” alisema wakati akizungumza na Mwananchi wakati walipomaliza darasa la saba

TANZIA: Mzee aliyebuni na kuchora Nembo ya Taifa AFARIKI Dunia

Mangufuli Awataka Wananchi Wampe Ushirikiano IGP Simoni Sirro

Aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Ernest Mangu amewataka wananchi kumpa ushirikiano IGP mpya, Simon Sirro katika kukabiliana na matukio ya uhalifu nchini hasa katika Mkoa wa Pwani.

Mangu aliyasema hayo jana  Ikulu jijini Dar es salaam baada ya Rais John Magufuli kumwapisha Sirro kuwa IGP mpya wa kuliongoza jeshi la polisi nchini.

Kuhusiana na hali inayoendelea mkoani Pwani, Mangu alisema "Sirro anafahamu anachotakiwa kufanya katika hilo, nimefanya naye kazi kwa karibu, ninachoomba ni askari na wananchi wote wampe ushirikiano"

Mangu ambaye anasubiri kupangiwa kazi nyingine alisema anamfahamu Sirro kama mchapakazi mzuri na ataweza kutekeleza majukumu yake ya kuhakikisha kwamba Tanzania inakuwa na amani.

Sirro aliapishwa jana kuwa IGP, kabla ya uteuzi huo alikuwa kamanda wa polisi (RPC) katika mikoa ya Tanga, Mwanza na Shinyanga. 
Baadaye alikwenda kitengo cha operesheni na mafunzo polisi makao makuu, kisha akahamishiwa kitengo hicho kanda maalumu ya Dar es Salaam kabla ya kuwa kamishna wa kanda hiyo.

Ole MedeyeOle Medeye Ajitumbua mwenyewe Nafasi ya Kaimu Katibu Mkuu UDP

Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha 'The United Democratic Party' (UDP) ametangaza rasmi kujiuzulu nafasi hiyo kwa madai ya kujipa fursa ya kuitumikia familia yake.

Ole Medeye ambaye alijiunga na UDP akitokea CHADEMA mapema mwaka jana, ametoa kauli hiyo jana katika barua aliyomuandikia Mwenyekiti wa chama hicho Mh. John Cheyo, huku akimshukuru kwa kumuani katika nafasi hiyo kwa kipindi chote.

"Napenda kukujulisha rasmi kwamba ili nipate muda wa kutosha kufanya shughuli za ustawi na maendeleo ya familia na jamii inayonitegemea nimeamua kwa hiari yangu kujiuzulu nafasi hiyo ya Katibu Mkuu kuanzia tarehe ya barua hii".Imesema sehemu ya barua hiyo

Mwanasiasa huyo amewahi kushika nyazifa mbalimbali ikiwemo Ubunge wa Jimbo la Arumeru Magharibi kupitia CCM katika Bunge la 10 na kupitia nafasi hiyo aliweza pia kuwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi katika serikali ya awamu ya nne.

Mara baada ya kushindwa katika kinyang'anyiro cha ubunge wa jimbo hilo katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, aliamua kuhama chama na kujiunga na CHADEMA ambapo hakudumu sana licha ya CHADEMA kumpa nafasi ya kugombea nafasi ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kisha alihamia UDP kabla ya kupewa nafasi ya Kaimu Katibu Mkuu wa chama hicho.

Baba Amkata Amkata Makalio Mwanaye

Mwanamume mmoja mkazi wa Ndofe wilayani Nyamagana mkoani Mwanza amemfanyia kitendo cha ukatili mtoto wake kwa kumkata na kisu sehemu za makalio kwa madai ya utoro shuleni.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza DCP Ahmed Msangi amemtaja mtuhumiwa huyo kuwa ni Nuhu James (50) anayedaiwa kumfanyia ukatili mtoto Ndalo Nuhu (14) ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha pili Shule ya Sekondari Igoma kwa kumfunga kamba miguuni na mikononi kisha kumchapa fimbo sehemu mbalimbali za mwili wake na baadaye kumkata na kisu sehemu za makalio, tukio analodaiwa kulifanya majira ya saa 11:00 alfajiri ya tarehe 25 Mei, 2017.

Inadaiwa kuwa mtuhumiwa aliaamua kumfanyia ukatili wa aina hiyo mtoto wake baada ya kugundua kwamba mwanaye ni mtoro shuleni.

Kamanda Msangi amesema baada ya mama wa mtoto alipoona ukatili anaofanyiwa mwanaye na hali yake kiafya kuzidi kubadilika alishindwa kuvumilia na arehe 28 Mei.2017 aliamua kutoa taarifa kituo cha polisi

Kamanda Msangi ameendelea kusema kuwa polisi wapo katika upelelezi na mahojiano na mtuhumiwa pindi uchunguzi utakapokamilika, mtuhumiwa atafikishwa mahakamani huku majeruhi akipelekwa hospitali kwa ajili ya matibabu na hali yake inaendelea vizuri.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne ya May 30

Jumatatu, 29 Mei 2017

Nape Awaponda Wabunge Wanaoisifia Serikali kwa Kila Kitu

Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye amefunguka na kusema wabunge wa Chama Cha Mapinduzi ambao wanaishauri na kuikosoa serikali ni watu ambao wana mapenzi mema na Rais na serikali yake kuliko wanao sifia kila kitu.

Nape Nnauye amedai wabunge ambao kazi yao ni kusifia kila kitu hata kama kuna mapungufu hao hawana mapenzi ya kweli kwa Rais Magufuli na serikali kiujumla na kudai yeye anaitumia nafasi yake vizuri kutoa ushauri kwa serikali kupitia bunge sababu ndiyo njia sahihi aliyonayo kwa sasa.

"Kimsingi kazi kubwa ya Mbunge hasa wabunge wa CCM ni kuishauri serikali yake sisi tunaoshauri tunampenda zaidi Rais na tunaipenda zaidi serikali ifanye vizuri kuliko wale ambao watakuja na kusifu na kupongeza kwa kila kitu, hata pale wanaona kabisa hapa tungeweza kushauri na mambo yakarekebishika" alisema Nape Nnauye

Mbali na hilo Nape Nnauye amedai kuwa watu ambao wanashangaa yeye kuishauri serikali sasa kupitia bunge anasema hawafahamu pia alipokuwa kwenye Baraza la Mawaziri, alikuwa akifanya hivyo.

Wanaosafiri kati ya Tanzania na DRC kupimwa Ebola, Waziri Ummy aeleza hali ya ugonjwa huo nchini.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Ally Mwalimu amesema mpaka sasa hakuna mgonjwa wa Ebola wala anayehisiwa kuwa na virusi vya ugonjwa huo nchini Tanzania huku Tsh. bilion 1.5 zikiwa zimetumika kuukabili ugonjwa huo
 
Ummy amebainisha hayo leo wakati alipokuwa anazungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam na kusema wananchi wasiwe na hofu ila wanapaswa kuchukua tahadhari huku akisisitiza kuwa wameweka kifaa maalum 'register' ambacho kitawalazimu wasafiri wote kujaza wakiwa wanakwenda  katika nchi ya DRC na pindi wakiwa wanatoka huko kuingia nchini.

"Hadi sasa hakuna mgonjwa hata mmoja wa Ebola wala mwenye virusi Tanzania, tumechukua tahadhari katika mikoa yote inayopakana na nchi ya Congo DRC. Wasafiri wote wanaotoka DRC wakifika Tanzania lazima waandikishwe kimaalum ili kufuatiliwe kama huko alikotoka hali ikoje na kama hana virusi nyemelezi. Tunawaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza katika kuwapima wasafiri wote kwenye mipaka yetu na Congo DRC" alisema Ummy.

Aidha, Ummy amesema serikali imeagiza mashine nne za nyongeza kutoka nje ya nchi ili kuongeza nguvu ya upimaji wa virusi vya ugonjwa huo.

Diamond: Sitaki Tiffah awe msanii, naogopa ataliwa sana na Wanaume

Diamond Platnumz amefunguka kwa kudai kuwa hataki mtoto wake wa kike Tiffah awe msanii kwa madai akiwa msanii atatembea kimapenzi na wanaume wengi.

Muimbaji huyo amedai mtoto wake huyo akiwa msanii, wanaume wengi watamiminika kumtaka kimapenzi.

“Mtoto wangu wa kiume ningependa awe msanii lakini mtoto wangu wa kike sitaki awe msanii, watamla sana,” alisema Diamond weekend iliyopita  akiwa katika kipindi KTN nchini Kenya. 

“Mtoto akiwa msanii watu wanaomjua wanakuwa wengi, watu wanaokujua wakiwa wengi na kutongozwa kunakuwa kwingi, sasa watanipa presha,”

Aliongeza, “Ukiwa mwanaume lijali na ukiwa kwenye nafasi kama yangu lazima wataliwa. Nilikuwa kwenye kutafuta tafuta, mpaka nilivyompata Zari na kweli nimetulia,”

Muimbaji huyo Jumanne hii anatarajia kuhudhuria mazishi ya aliyekuwa mume wa Zazi, Ivan aliyefariki wiki iliyopita nchini Afrika Kusini kwa ugonjwa wa moyo.

Watoto Saida na Wilson wameruhusiwa kutoka Hospital Mercy Marekani

Majeruhi  wa ajali  ya gari iliyohusisha vifo 35 vya wanafunzi, walimu pamoja na dereva wa shule ya msingi Luck Vicent  wilayani Karatu, Watoto Sadia na Wilson pamoja na wazazi wao wakiwa kwenye gari maalum ya wagonjwa baada ya kuruhusiwa kutoka hospitali ya Mercy Marekani ambapo walipelekwa kwa matibabu zaidi.

Hii ndiyo sababu ya Magari ya wanafunzi kuwa na rangi ya Manjano

Inasemekana kuwa Sababu ya mabasi ya shule kuwa na rangi ya njano ni kuepusha ajali, binadamu anaona rangi ya njano haraka kuliko rangi nyingine. Ili kuepusha ajali ndo maana magari mengi ya wanafunzi hapa duniani yanatambulika kwa kupakwa rangi  ya manjano

Kamanda Sirro Aapishwa Rasmi Kuwa IGP Mpya

Rais John Magufuli amemuapisha mkuu mpya wa Jeshi la Polisi nchini, Simon Sirro aliyeteuliwa jana kuchukua nafasi ya Ernest Mangu.
 
Hafla hiyo imehudhuliwa na viongozi mbalimbali akiwemo Makamu wa Rais, Samia Suluhu, Waziri wa Mambo ya Ndani , Mwigulu Nchemba na makamishna mbalimbali wa jeshi hilo.
 
Sirro baada ya kuapishwa amekula kiapo cha maadili mbele ya Rais Magufuli kwa ajili ya kutekeleza majukumu yake mapya.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu ya May 29