Powered by: Elbahsan Web & Blog Designer
Do want your Network!!! Website or Blog-Spot, Try Us: Elbahsan Web & Blog Designer Contact Us Now... Calll; +255743550360 | +255788680558 Email; murtadhaalbahsan@gmail.com

Zawamba Photo Production

Jumatatu, 26 Novemba 2018

Taarifa Toka Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais IKULU

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 26 Novemba, 2018 ameungana na Maaskofu, Mapadre, Watawa na Waumini wa Kanisa Katoliki kutoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Mbeya Mhashamu Askofu Evaristo Chengula aliyefariki dunia tarehe 21 Novemba, 2018 katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete Jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa Matibabu.

Misa Takatifu ya kumuaga Marehemu Askofu Chengula iliyoongozwa na Askofu Mkuu Mwandamizi Jude Thadaeus Ruwa’ichi, imefanyika katika Kanisa la Mtakatifu Imakulata lililopo Makao Makuu ya Baraza la Maaskofu, Kurasini Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa na Mkewe Mhe. Mama Anna Mkapa.

Akizungumza baada ya Misa hiyo Mhe. Rais Magufuli ametoa salamu za pole kwa Maaskofu wote wa Kanisa Katoliki, Mapadre, Watawa, Waumini wa Kanisa Katoliki Jimbo la Mbeya na Wakatoliki wote nchini kwa kuondokewa na kiongozi aliyekuwa akifanya vyema kazi yake ya kutangaza Injili.

Mhe. Rais Magufuli amesema pamoja na majukumu yake ya kutoa huduma za kiroho Marehemu Askofu Chengula alisimamia ukweli ikiwemo kupinga hadharani ndoa na mapenzi ya jinsia moja licha ya kuwepo mashinikizo mbalimbali.

Akitoa salamu kwa niaba ya Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) Makamu wa Rais wa TEC Mhashamu Askofu Flavian Kasalla amemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa ushirikiano alioutoa wakati wa kuuguza na baada ya kifo cha Askofu Chengula na pia amewashukuru madaktari na wauguzi, viongozi na wote waliokuwa wakimuombea kabla na baada ya kifo.

Mhashamu Askofu Evaristo Chengula amefariki dunia kwa ugonjwa wa moyo na baada ya Misa ya kumuaga mwili wake umesafirishwa kwenda Mbeya.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
26 Novemba, 2018

ZAIDI YA MADEREVA 1600 WAPATIWA MAFUNZO ARUSHA


Mrakibu wa polisi Joseph   Charles Bukombe mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani  mkoani Arusha 

Na. Vero Ignatus, Arusha


Madereva wa mabai ya kubebea abiria katika mkoa wa Arusha wamepatiwa mafunzo ilihali wengine waki3ndelea na mafunzo


Akizungumza  Mrakibu wa polisi Joseph   Charles Bukombe mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani  mkoani Arusha amesema lengo kuu ni kuhakikisha kuwa madereva wote wanapata elimu na wanatoa huduma inayoendana na elimu waliyoipata


Tangia kuanzishwa kwa mafunzo ya madereva miezi minne iliyopita madereva 1600 wamehitimu mafunzo wa magari ya kubeba abiria  (PSV)kupitia chuo cha Veta pamoja na chuo rafiki wa NIT cha Moden driving vyote vya mkoa wa Arusha.


 "Pamoja na mapambano hayo ya ajali za barabarani ni  lazima kuhakikisha kuwa wapo madereva wenye weledi" alisema Bukombe. 


Aidha amesema mafunzo haya yamesaidia sana kwani mkoa hapo pamekuwa salama bila Ajali  


"Tangia tumeanzisha mafunzo takribani miezi minne iliyopita kwa mkoa wa Arusha tupo salama, na ukikuta ajali imesababishwa na bodaboda na siyo magari ya abiria" alisema Bukombe


Mara baada ya kuona ajali zimeongezeka jeshi la polisi liliendesha ukaguzi wa leseni na kugundua kuwa madereva wengi wana leseni lakini hawana vyeti, kwahiyo yamkini wanazipata leseni kwa njia wanazozijua wao


"Sisi tukasema hawawezi kuendelea na leseni walizonazo badala yake warudi darasani kwenda kusoma ili waweze kupata vyeti"alisema


Akizungumza wimbi  la Magari ya viongozi wa serikali kupata ajali Bukombe amesema hakuna aliye juu ya sheria kwani hata madereva  hao wameshaanza kushughulikiwa

"Mara ya kwanza ulipita tu kama upepo wa kuwasaha ulakini sasa unapoaona kitu kinazidi kuleta shida ule upepo tumeshafutilia mbali na wao wanachukuliwa hatua "alisema


Amesema Jeshi la polisi linafikiria ninamna gani wanaweza kushirikiana na wizara kuhakikisha madereva wao wanawapeleka mafunzoni


Aidha Bukombe ametoa wito kwa madereva wakaidi ambao hawaoni umuhimu wa kuingia darasani, wale ambao wanasubiri waone ninini hatima ya jambo hilo amewashauri kuw ni  vyema wakarudi darasani kujisomea wasisibirie matokeo kwani jeshi la poisi hatitawafumbia macho.


Bikombe amesema maelekezo hayo yalipoyolewa na serikali yalikuwa ni kwa minubu wa miezi mitatu ambapo zoezi hilo likikuwa limalizike tarehe 1 novemba 2018, ikaonekana vyuo vilelemewa na maderevya hivyo serikali ikaongeza hadi miezi miwili hivyo litamalizika januari mosi 2019

Ukaguzi wa leseni na vyeti utaendeshwa rasmi januari mosi 2019 hivyo madereva ambao watakutwa hawana leseni na vyeti sheria itafuata mkondo wake.

Polisi Anayetuhumiwa Kubaka Mtoto wa Miaka 13 Akosa Dhamana

Ofisa wa Jeshi la polisi mstaafu Mashaka Mdachi (72) amefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Morogoro kujibu shitaka la kumbaka na mwanafunzi wa darasa la tano mwenye miaka 13.

Mbele ya hakimu wa mahakama hiyo Elizabert Nyembele, mwanasheria wa Serikali Mary Lundu alidai mshtakiwa alitenda kosa hilo kati ya Januari 2017 na Oktoba 2018 katika nyakati tofauti huko Area Five kata ya kichangani Manispaa ya Morogoro.

Mwanasheria huyo alidai mahakamani hapo Ijumaa ya Novemba 23, 2018 kuwa mshtakiwa alifanya kitendo hicho huku akijua ni kosa kisheria na kumuathiri kisaikolojia binti huyo.

Alipotakiwa kujibu shitaka hilo mshtakiwa huyo alikana na mahakama Iliahirisha kesi hadi Desemba 6, 2018 itakapotajwa tena wakati polisi wakiendelea na upelelezi wa kesi hiyo na mshtakiwa alipelekwa rumande baada ya kukosa wa kumdhamini.

Watatu Washikiliwa Na Jeshi La Polisi Kwa Kukutwa Na Nyara Za Serikali

Na. Vero Ignatus, Manyara
Jeshi la polisi Mkoani Manyara, linawashikilia watu watatu kwa kudaiwa kukutwa na nyara za serikali ikiwemo vipande vitatu vya jino la Tembo.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Manyara, Augostino Senga akizungumza jana alisema watu hao walikamatwa kwenye nyumba ya kulala wageni ya Top In One iliyopo mtaa wa Oysterbay mjini Babati.

Kamanda Senga aliwataja watu hao kuwa ni Anthony Paschal (28) na Juma Ingi wote wakazi wa Endasak wilayani Hanang' na Tluway Gosi mkazi wa Simbay wilayani Hanang'. Alisema mbinu waliyotumia ni kuficha vipande hivyo ndani ya mfuko wa sulphate kisha kuweka chini ya uvungu wa kitanda ili wakaiuze.

Alisema baada ya timu ya makachero kwa kushirikiana na maofisa wanyamapori wa shirika la hifadhi ya Taifa ya Tarangire kupata taarifa walifika eneo hilo na kuwakamata watu hao. "Watuhumiwa hao wote wanashikiliwa na polisi na tunaendelea na upelelezi kabla ya kuwafikisha mahakama kwa ajili ya kujibu mashtaka yanayowakabili," alisema kamanda Senga.

Katika tukio lingine, kamanda Senga alisema watu watatu wanashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kukutwa na lita 40 za pombe haramu ya moshi maarufu kama gongo. Alisema watu walikamatwa juzi kwenye kijiji cha Kazamoyo kata ya Kisangaji wilayani Babati wakiwa wamebeba kwenye pikipiki aina ya Skygo yenye namba za usajili MC 970. Aliwataja watu hao kuwa ni Daniel Hewasi (47) mkazi wa Magugu, Hussein Athuman (50) mkazi wa kijiji cha Kazaroho na Idd Hamis (35) mkazi wa kijiji cha Magugu.

Alisema watu hao walikuwa wamebeba pombe hiyo haramu kwenye pikipiki hiyo wakiwa wamehifadhi kwenye madumu mawili ya lita 20 kila moja.Alisema pikipiki hiyo iliyokuwa imebeba pombe hiyo haramu ni mali ya Idd Hamis na lengo lao ilikuwa ni kwenda kuuza ili kujipatia kipato.

Alisema polisi wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo kabla ya kuwafikisha mahakamani wakajibu mashtaka yanaoyowakabili.

Sheria mpya ya Mafao: SSRA watoa ufanunuzi

 
Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii SSRA, kupitia Mkurugenzi Mkuu, Irene Isaka, imekanusha malalamiko ya kupunguzwa kwa mafao ya wastaafu kupitia kanuni mpya za mwaka 2018 na kudai kuwa, taratibu zinazotumika ni za mwaka 2014.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam, Irene Isaka amesema changamoto hiyo inasambazwa na wanachama wachache, pia ni jambo ambalo linaweza kuzungumzika na kuongeza kuwa sheria ambayo imepitishwa inalenga kuifanya mifuko hiyo pamoja ili ilete faida kwa wanachama wake.

“Sheria ya kuunganisha mifuko imeleta usawa wa wanachama, kwa viwango wanavyochangia, kupunguza gharama za uendeshaji, jambo lingine ni kuweka uwaniano kati ya wachangiaji na wastaafu, lakini sasa tuna uwiano mzuri, pia sasa hivi hata akifariki mafao yataendelea kwa miaka 3,” amesema Kisaka.

Isaka ameeleza kuwa, haikuwa sahihi kundi dogo kulipwa mkupuo mkubwa wa zaidi ya mara tatu ya michango aliyochanga kwa kipindi chote cha ajira yake tofauti na wenzao hivyo, asilimia 25% iliyopunguzwa kwenye mkupuo imewekwa kwenye pensheni ya kila mwezi ambayo imeongezeka kwa asilimia 50%.

“Sheria hii imetatua changamoto, kwa hiyo niwaondoe wasiwasi lengo ni zuri na hata wanaolalamika ni wachache kwa sababu tunawastaafu zaidi ya laki moja kwa hiyo ni sehemu ndogo ya wanachama wenye hofu,” ameongeza.

“Kuhusu wategemezi wameshalipwa wengi, kwa sheria mpya imeongeza mafao na maslahi kwa wanachama wetu, ndiyo maana watu wengine kutoka nchi za Burundi, Namibia wamekuja kujifunza kwetu kwa sababu tumefuata vizuri kanuni za shirika la kazi duniani 'ILO'.”

Novemba 22 mwaka huu, Mbunge wa Bunda, Ester Bulaya alisema “tuliwaambia dhamira ya kuunganisha mifuko ya hifadhi ya jamii ilikuwa ni serikali kukwepa madeni inayodaiwa na mifuko ya hifadhi ya jamii ambayo kwa sasa inafikia trilioni 8 kwa sababu waliwekeza kwenye miradi isiyokua na tija,”

Ukichumbia, Ukioa au Kumpa Mimba Mwanafunzi Jiandae Kuzeekea Jela

 
Serikali imesema imebadili utaratibu gerezani kwa watu watakaotumikia kifungo cha miaka 30 jela kutokana na kuwapa mimba au kuoa mwanafunzi.

Utaratibu huo uliobadilishwa ni wa kuhesabu siku, ambapo sasa mfungwa wa makosa hayo atahesabiwa usiku na mchana kuwa ni siku moja badala ya usiku na mchana kuwa siku mbili ilivyo kwa wafungwa wengine.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ndiye aliyefichua suala hilo jijini hapa jana, alipozindua Kampeni ya Siku 16 Kupinga Ukatili wa Kijinsia ambayo hufanyika kila mwaka kuanzia Novemba 25 hadi Desemba 10.

Kampeni hiyo imeratibiwa na Shirika la Wanawake katika Sheria na Maendeleo Barani Afrika (WiLDAF) kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo.

Akizungumza na wananchi katika uzinduzi huo, Majaliwa alisema serikali imewezesha marekebisho ya Sheria ya Elimu na kulifanya kosa la kumpa mimba kuoa au kuolewa mwanafunzi kuwa kosa la jinai na pale inapothibitika, adhabu yake ni kifungo cha miaka 30, hivyo watakaokutwa na mkono wa sheria "watakiona cha mtema kuni".

“Huwa nalizungumza hili, mtu yeyote atakayekutwa na tukamkamata amempa mimba, amemuoa, amemchumbia mwanafunzi, adhabu yake ni kubwa sana na kabla hujafanya tendo hilo jiulize una miaka mingapi ili ujue utakapoadhibiwa ukajumlisha na miaka yako tuone ukienda gerezani ujue unatoka na miaka mingapi," Majaliwa alisema na kuongeza:

"Kule gerezani tumesema utaratibu wa kuhesabu mchana na usiku kuwa ni siku mbili, kwenye adhabu hii ni siku moja tu, kama ni miaka 30 basi miaka 30 kweli, sasa je, miaka 30 utarudi ukiwa hai wewe?"

Waziri Mkuu aliwataka Watanzania kuwa macho na wale wote wasiowatakia mema wanafunzi, akiagiza kuwa "mtu akikutwa amesimama kwenye kona isiyoeleweka na mwanafunzi ashughulikiwe."

“Na wale wataalamu wa kuwasalimia wanafunzi mara nne nne kwa siku, ole wako tukikukamata utakiona cha mtema kuni, kwa hiyo eneo hili tumeimarisha kumlinda mtoto wa kike na serikali ya awamu ya tano imewekeza kwa mtoto wa kike," alisema.

Alisema mpango wa kufikia asilimia 50 kwa 50 utafikiwa kama ikiwekezwa kwa mtoto wa kike na serikali imedhamiria kufikia hatua hiyo.

Majaliwa alisema ukatili wa kijinsia hususan dhidi ya wanawake na watoto unarudisha nyuma juhudi za serikali za kuhakikisha kuwa mapinduzi ya viwanda na kilimo yanafikiwa.

“Hatuwezi kuwa na taifa linalozalisha na kufikia malengo ya kuwa nchi ya uchumi wa kati iwapo muda mwingi unatumika kuamua migogoro na kuhudumia waathirika wa ukatili wa kijinsia badala ya kushiriki katika shughuli za uzalishaji,” alisema.

Aliwaagiza wakuu wa mikoa kuhakikisha wanasimamia uanzishwaji wa kamati za ulinzi wa wanawake na watoto kwenye mikoa, halmashauri, kata na vijiji kama ilivyoelekezwa kwenye mwongozo wa uratibu wa mpango wa taifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

“Nawaagiza wakurugenzi wa halmashauri zote kuanzisha programu za kijamii za kutokomeza ukatili wa kijinsia katika halmashuari husika zitakazozingatia hali halisi na kuzitengea bajeti programu hizo," alisema.

Majaliwa pia aliwataka wadau kutumia siku hizo kuwasilisha mapendekezo kama kuna upungufu unaohitaji sheria zitungwe kuwasilisha kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa ajili ya kutunga sheria.

Waziri Mkuu pia alisema kumekuwa na matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii yanayoleta madhara kwa jamii.

Aliagiza kila taasisi na kampuni ya simu kuhakikisha inawachukulia hatua kali dhidi ya watakaobainika wanatumia vibaya mitandao ambayo inarudisha nyuma jitihada za kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia.

“TCRA (Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano) ambao ndiyo wanaofuatilia watumiaji wote wa mitandao, hakikisheni mnadhibiti na wale wote mnaojidanganya kuwa kuna mitandao haionyeshi, tukikukamata ndio utajua kuwa tunakuona," alisema.

Wakosa Dhamana kwa Mara ya Tatu: Amber Rutty na Mpenzi wake Warudishwa tena Segerea

 
Msanii Rutyfiya Abubakary maarufu kama ‘Amber Ruth’ na mpenzi wake Said Bakary Kitomali wamekosa tena dhamana kwa mara ya tatu katika kesi inayowakabili ya kufanya mapenzi kinyume na maumbile.

Mbali na Amber Ruth na Said Bakary, mshtakiwa mwingine ni James Charles maarufu kama ‘James Delicious’ ambaye yeye yupo nje kwa dhamana.

Mshtakiwa Amber Rutty alimueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Augustine, Rwezire kuwa mdhamini wake mmoja amefika mahakamani hapo lakini mwingine bado hajafika.

Baada ya kueleza hayo, Hakimu Rwezire amemwambia Amber Rutty kwamba dhamana ipo wazi na shughuli za mahakama zinaisha saa 9 alasiri hivyo wadhamini wake wakikamilika atadhaminiwa.Kesi imeahirisha hadi December 10,2018.

Katika kesi hiyo kosa la kufanya mapenzi kinyume na maumbile linamkabili Amber Ruth, ambapo anadaiwa amelitenda kati ama baada ya October 25, 2018 ambapo alimruhusu Said Bakary kumuingilia kinyume na maumbile, kosa ambalo amelikana.

Pia kosa jingine la kufanya mapenzi kinyume na maumbile, linamkabili mshtakiwa wa pili Said Bakary ambapo anadaiwa kati ama baada ya October 25,2018 jijini Dar es Salaam alifanya mapenzi na Amber Rutty kinyume na maumbile ambapo alisema si kweli.

Kosa la tatu la kuchapisha video ama picha za ngono, ambapo linamkabili James Charles ama James Delicious akidaiwa kati ya October 25,2018 alisambaza video za ngono kupitia magroup ya Whatsapp.

Kosa jingine la nne ni kusababisha kusambaa picha za ngono linamkabili Amber Ruth na Said Aboubakary ambapo wanadaiwa kati October 25,2018 walisababisha kusambaza picha za ngono kupitia makundi ya Whatsapp. Kosa ambalo wamesema si kweli.

Ili Amber Rutty na mpenzi wakewadhaminiwe wanatakiwa kutimiza masharti ya kuwa na wadhamini 2 ambapo kila mtu atasaini bondi ya Shilingi Milioni 1

Alichokisema Skauti Mkuu Mwantumu Mahiza Baada ya Kuapishwa Oktoba 3 na Rais Magufuli

Skauti Mkuu wa Chama cha Maskauti Tanzania, Mwantumu Mahiza ameahidi kujenga maadili ya vijana wa kitanzania.

Mahiza ameyaahidi hayo tarehe 3 Oktoba 2018 baada ya kuapishwa mbele ya Rais John Magufuli ikulu jijini Dar es Salaam.

Katika hatua nyingine, Mahiza ameahidi kuieneza skauti katika vyuo vya kati na vyuo vikuu

“Nakushukuru kwa kuniteua kulea vijana wa Tanzania kupitia skauti, wajibu wangu ni mambo mawili, kuhakikisha skauti inaenea katika vyuo vya kati na vyuo vikuu kwa sababu miaka mingi ilienea shule za msingi na sekondari,” amesema Mahiza.

Vile vile, Mahiza ameahidi kufanikisha ujenzi wa kambi ya kimataifa ya Skauti jijini Dodoma.

“Wajibu wangu wa pili, ni kuhakikisha tunafanikisha ujenzi wa kambi ya kimataifa jijini Dodoma. Nakuahidi sitakuangusha,” amesema.