Powered by: Elbahsan Web & Blog Designer
Do want your Network!!! Website or Blog-Spot, Try Us: Elbahsan Web & Blog Designer Contact Us Now... Calll; +255743550360 | +255788680558 Email; murtadhaalbahsan@gmail.com

Zawamba Photo Production

Ijumaa, 2 Desemba 2016

SKAUTI WAFANYA ZIARA IPP MEDIA


Skauti wakiwa katika chumba cha habari cha magazeti ya The Guardian



Na Rehema Ramadhani
Dar es salaam; Chama cha Skauti Tanzania kiliambatana na Skauti kutoka Poland, Kenya na Burundi ambao ni washirki wa mafunzo maalum ya Public Relation, mapema jana 1/12/2016  walifanya ziara na kujione kazi mbalimbali zinazofanywa na kampuni ya IPP Media iliyopo Mikocheni Jijini Dar es Salaam.


Akizungumza na wanachama wa Skauti Tanzania, Msemaji wa  Chumba cha Habari Magazeti ya The Guardian na Nipashe  Bw. Faustin Felisian amesema wamefarijika na ujio huo wa wanachama kutoka Skauti kwa kuja kujifunza na kuona jinsi gani habari zinavyoandaliwa mpaka gazeti linapotoka mitaani.
“Tumefarijika sana kwaujio wenu katika chumba chetu cha Habari kwani ni jambo jema kujifunza na natumai wapo amabo watavutiwa na vinavyofanyika na wengine watatamani kuwa wana habari hapo baadae” alisema Bw. Felisian

Mmoja wa wanachama wa Chama cha Skauti Tanzania Ndg. Murtadhwa Rashid amesema kuwa ziara hiyo katika chombo cha habari imekuwa ya mafanikio na faida kwao kwani wamepata fursa ya kujionea mambo mbalimblai yahusuyo uandishi wa habari.
“Tumefurahi kwa kupata elimu na tumepokelewa vizuri  IPP Media. Tuna mipango ya kuifikisha Skauti yetu mbali kwa malengo ya vijana wa Taifa letu na tunawakaribisha watu wote waje kwenye uskauti tujifunze kwa pamoja” Alisema Ndg. Murtadhwa Rashid .

Picha na Nelson Opany na Ausi Hussein






This Blog Powerd by:
  Elbahsan Web & Blog Designer
A Subsidiary of  Elbahsan Web & Blog Designer for Global Development, Inc.
+255 (0) 653 373 432 & +255 (0) 778 246 889
For the Web & Blog Template and Designing
Dar Es Salaam, Tanzania
 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni