Powered by: Elbahsan Web & Blog Designer
Do want your Network!!! Website or Blog-Spot, Try Us: Elbahsan Web & Blog Designer Contact Us Now... Calll; +25565373432 | +255778744123 Email; murtadhaalbahsan@gmail.com

U-RREPORT TANZANI (TSA)

ZAMZAM GIRLS ISLAMIC SEC SCHOOL

Zawamba Photo Production

Jumapili, 11 Februari 2018

WATENDAJI WA ARDHI WAZIMIA BAADA YA KUSHINDWA KUTOA MAJIBU KWA RC MAKONDA

Watendaji wa Ardhi wa Manispaa za Jiji la Dar es salaam leo *wamejikuta kwenye wakati mgumu* baada ya kupata *kigugumizi na kushindwa kujibu maswali ya msingi* yaliyokuwa yakiulizwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam *Mhe. Paul Makonda* kuhusu idadi ya *Migogoro ya Ardhi* katika idara wanazoongoza na kusababisha baadhi yao *kudondoka kwa kuzimia na kukimbizwa hospital.*

Kitendo cha *wakuu hao wa idara* kushindwa kujibu *maswali* ambayo yamekuwa chanzo cha *migogoro ya ardhi* isiyoisha *kimewakera Maelfu ya wananchi* waliojitokeza kwenye ukumbi wa *Diamond Jubilee* kwaajili ya kujua *hatma ya Malalamiko* yao na kujikuta wakuomba *RC Makonda* kuwatumbua.

Kutokana na watendaji hao kushindwa kutekeleza majukumu yao *RC Makonda* ameagiza *wakuu wa idara ya ardhi Manispaa za Ubungo na Ilala* wapangiwe kazi nyingine kutokana na *kushindwa kutekeleza majukumu yao.*

Aidha *RC Makonda* amesimamisha shughuli zote za *Mabaraza ya Kata Dar es salaam* kuwakuwa hazina *uwezo wa kusikiliza kesi* na pia hawana *wataalamu wa sheria* kitendo kinachochangia *Migogoro mingi ya Ardhi*.

Kutokana na hilo *RC Makonda* amewataka *Makatibu Tarafa* kuanza kutembelea Mabaraza hayo kuanzia Jumatatu ya *February 12.*

*RC Makonda* amechukuwa uamuzi huo wakati wa kupokea *Ripoti ya Malalamiko ya Wananchi* waliodhulumiwa Haki zao ambapo zaidi ya *Wananchi 11,652* walifika kwaajili ya kupata *Msaada wa kisheria* ambapo jumla ya *malalamiko 3,373* yalipokelewa na kusikilizwa huku *wananchi waliosikilizwa wakiwa ni 6,052* na ambao hawakupata fursa ya kusikilizwa wakiwa ni *Wananchi 5600* ambapo leo *RC Makonda* ameandaa utaratibu wa kuhakikisha *wote wanasikilizwa.*

*RC Makonda* amesema *idadi kubwa ya wananchi* waliokimbilia kwake kutafuta haki ni tafsiri tosha kuwa *baadhi ya watendaji hawasimami ipasavyo* katika nafasi zao ambapo amewaagiza *Wakurugenzi kuanza kupitia wasifu wa wakuu wa idara CV na kazi zote wanazofanya.*

Ili kuhakikisha wanyonge walioporwa haki zao wanazipata *pasipo kuvunja sheria RC Makonda* amewasilisha kwa Kamanda wa Polisi kanda maalumu ya Dar es salaam *Majina ya watu wenye michezo ya kudhulumu wananchi* kwaajili ya kuchukuliwa *hatua za kisheria.*

*Makonda* ameagiza Watendaji kuhakikisha malalamiko yote ya wananchi ya *Migogoro ya ardhi, Mirathi,Talaka, Madai, Makosa ya jinai, Masuala ya kazi, Ubakaji na utapeli* yanafanyiwa kazi kabla ya mwezi April.

Aidha amewataka *madalali wote wanaofanya kazi ya kutekeleza hukumu za Mahakama au Bank* kufika ofisini kwake siku ya jumanne wakiwa na *nyaraka za usajili.*

Nao baadhi ya Wananchi waliofika kwenye mkutano huo *wamefurahia* hatua za *RC Makonda* katika kuwajali *wananchi wanyonge* ambapo pia wameshukuru *mkutano huo umewasaidia kujua kwa undani masuala ya kisheria*.

Aidha wamesema kuwa wanaamini kwa ujasiri *RC Makonda* wanafarijika kuona *tabu waliyoipata kwa miaka mingi wakitafuta haki yao inaenda kupatikana*.

*HUU NDIO UONGOZI THABITI UNAOACHA ALAMA, PONGEZI KWAKO RC MAKONDA*

Jumapili, 4 Februari 2018

Wafanyakazi waanza kukatwa mishahara kufadhili uchaguzi wa 2020


Wafanyakazi wa umma nchini Burundi wameanza kukatwa asilimia 10 ya mishahara yao kwaajili ya kufadhili uchaguzi mkuu unaotarajiwa mwaka 2020.

Katika kipindi cha miaka miwili ijayo, raia wote wa Burundi walio na zaidi ya umri wa kupiga kura wa miaka kumi na minane na zaidi, ni sharti wachangie katika hazina hiyo ya kitaifa.

Serikali ya Burundi imesema imechukua uamuzi huo ili kuziba pengo lililosababishwa na uamuzi wa wafadhili wa kuzuia misaada tangu mzozo wa mwaka 2015 wakati rais Pierre Nkurunziza alipowania muhula wa tatu.

Hata hivyo serikali imekariri kuwa hazina hiyo ya uchaguzi ni wazo la raia wa Burundi wenyewe, pendekezo ambalo limepingwa na wakuu wa vyama vya wafanyakazi.

NDALICHAKO: MLITUELEWA VIBAYA, MICHANGO SHULENI INARUHUSIWA

Jumanne, 9 Januari 2018

BUGURUNI: Bomba la Gesi lalipuka na kusababisha moto mkubwaTPDC imesema bomba la gesi limelipuka eneo la Mnyamani, Buguruni baada ya wafanyakazi wa Dawasco kulitoboa kwa bahati mbaya wakati wakitengeneza bomba la maji #MwananchiUpdates

Ikulu: Rais Magufuli akutana na Edward Lowasa Waziri Mkuu Mstaafu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 09 Januari, 2018 amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Edward Ngoyai Lowassa, Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Baada ya mazungumzo hayo Mhe. Edward Ngoyai Lowassa amempongeza Mhe. Rais Magufuli kwa kazi nzuri anayoifanya na ametaja baadhi ya maeneo ambayo kazi kubwa imefanyika kuwa ni kutoa elimu bila malipo, ujenzi wa mradi wa uzalishaji wa umeme katika maporomoko ya mto Rufiji (Stiegler’s Gorge), ujenzi wa viwanda na ujenzi wa reli kwa kiwango cha kisasa (Standard Gauge) ambavyo vinazalisha ajira nyingi kwa Watanzania.

“Nimepata faraja sana kuja hapa Ikulu kuonana na Mhe. Rais, tumezungumza nae na nimempongeza kwa kazi nzuri anayoifanya, lazima tukiri anafanya kazi nzuri na anahitaji kutiwa moyo.

“Moja kubwa ambalo ni la msingi sana ni la kujenga ajira, katika kuanza ujenzi wa reli ya kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro hapo anajenga ajira, na kwenye nchi yoyote inayoendelea suala muhimu ni kujenga ajira, Stiegler;s Gorge ni kujenga ajira na mingine ya aina hiyo, lazima kuwepo na kipaumbele cha kusema kwamba tunajenga ajira, jingine ni la elimu, ni muhimu sana, hauwezi kuacha elimu katika mambo yako unayofanya, hili nalo lazima lisemwe vya kutosha, kwa kweli nakushukuru Mhe. Rais, you made my day” amesema Mhe. Lowassa.

Kwa upande wake Mhe. Rais Magufuli amempongeza Mhe. Edward Ngoyai Lowassa kwa kutambua kazi kubwa inayofanywa na Serikali na amesema Mhe. Lowassa ni mmoja wa viongozi ambaye kwa wakati wake ametoa mchango wake katika nchi.

Mhe. Rais Magufuli ameongeza kuwa Mhe. Lowassa ni mwanasiasa mzuri kwani hata wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu uliopita ambao naye aligombea kiti cha Urais, hakuwahi kumtukana.

“Mhe. Lowassa ameniomba mara nyingi nikutane nae, na leo nimekutana nae, tumezungumza mambo mengi, ameniambia ya kwake na mimi nimemwambia ya kwangu, kwa ujumla Mhe. Lowassa ni mwanasiasa mzuri na tuendelee kuwaenzi wazee hawa ambao kwa nyakati fulani walifanya mambo mazuri, na mimi napenda kumpongeza Mhe. Lowassa ambaye kama alivyosema hapa kuwa tumefanya mambo mazuri mengi.

“Ametaja miradi mbalimbali tunayotekeleza, ametaja mradi wa Stiegler’s Gorge utakaogharimu zaidi ya Shilingi Trilioni 7, amezungumzia juu ya elimu bure, amezungumzia juu ya maji ambayo kwa bahati nzuri yeye alikuwa Waziri wa Maji na anafahamu sasa tumefikia wapi, amezungumza juu ya umeme tulivyosambaza katika vijiji mbalimbali, elimu bure, huduma za hospitali na mengine” amesema Mhe. Rais Magufuli.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
09 Januari, 2018

Jumatatu, 8 Januari 2018

BIG NEWS: VIBOKO 12 KWA ATAKAE SIMAMA NA MWANAFUNZI, NA FAINI .........

TAHADHARI
BAKORA ZITAKUHUSU


Kama wewe ni kijana wa kiume usisimame na wanafunzi wa like, ukionekana tu utachapwa viboko 12 au faini Tshs. 10,000

Ukiwa katika kata ya Ihungwe wilayani Sengerema usithubutu kusimama na mwanafunzi wa kike, ukikamatwa utachapwa viboko 12 au faini ya 10,000 baada ya viongozi wa kata hio kupitisha rasmi sheria hio  katika kikao chao cha baraza la maendeleo ya kata kilichofanyika hivi karibuni, kufuatia tatizo la kupata mimba wanafunzi wa kike kuzidi kuwa sugu.

Sheria hio  ndogo imepitishwa ikitanguliwa na agizo la Mkuu wa wilaya ya Sengerema Nd. Emanuel Kipole alieagiza Wanaume watakaokutwa na wanafunzi wa kike  wapigwe bakora 12 au faini ya Tsh.10,000, agizo hilo  alilitoa mwezi oktoba mwaka 2017

Chanzo: Gazeti la Mwananchi.

Jumapili, 7 Januari 2018

NEWS: CHAMA CHA SKAUTI TANZANIA CHAELEKEA KWENYE.........

CHAMA CHA SKAUTI TANZANIA CHAELEKEA KWENYE UCHAGUZI MKUUMAPEMA MWAKA HUU 2018.


Habari na, Murtadhwa Elbahsan.

Chama cha Skauti Tanzania kimetangaza upatikanaji wa fomu za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi, hii ni desturi ya upatikanaji wa uongozi wa Skauti Tanzania.

Kwa kupitia Mkutano Mkuu Maalum wa Baraza Kuu la Chama cha Skauti Tanzania, ambacho ndicho chombo kincho piga  kura na kupata viongozi WA juu wa chama hicho, Baada ya kukamilisha mhakato wa upatikanaji wa majina 3 ya skauti mkuu yatakayo pelekwa kwa Mlezi wa Skauti Tanzania ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuteua Skauti Mkuu.

"Kwa sasa chama cha skauti Tanzania kinataraji kufanya uchaguzi mkuu wa kupata viongozi wao wa juu, ambapo tarehe rasmi za uchaguzi huo ni 22 Februari 2018 katika ukumbi wa Karimjee" alisema Bi. Eline Kitaly ambaye ni Kamishna Mtendaji wa Skauti

Fomu rasmi ya kugombea nafasi ya skauti Mkuu hii hapa chini......


VIGEZO MAALUM VYA KUMPATA SKAUTI MKUU

Mwombaji awe na sifa zifuatazo:
1. Awe na umri usiopungua miaka 45
2. Awe kiongozi aliyewahi kutoa huduma iliyotukuka kwa
Chama cha Skauti Tanzania na Jamii
3. Awe na ueledi wa mambo ya Skauti
4. Awe miongoni mwa Wakufunzi Wasaidizi (ALTs)
5. Awe na uzoefu usiopungua miaka 15 katika uongozi wa
Skauti Watu Wazima (Adult in Scouting)
6. Awe na Uwezo wa kusimamia na kuendeleza Skauti kwa
ujumla


Eidha kwa sasa Bi. Mwantum B. Mahiza ndio Skauti Mkuu na Kamishna Mkuu wa Skauti ni Ndugu Abdulkarim E. H. Shah.

Chama cha Skauti pamoja na kuwa na Makamishna wakuu wa saidizi pia kuna Naibu Kamishna Mkuu ambaye ni ndugu Rashid K. Mchatta, viongozi wote hao wanamaliza muda wao wa uongozi tangu kuchaguliwa kwaomara baada ya kupatikana viongozi wapya baada ya uchaguzi na kfuatiwa kuteuliwa kwa Skauti Mkuu na Mlezi wa Skauti (Rais wa nchi)


Kipenga cha kumtafuta Skauti Mkuu kimepulizwa, nafasi ziko wazi na mwisho wa kurudisha fomu ni tarehe 15 Januari, 2018 waweza kujaza fomu kielektronik kwa kubonfya hapa >>>>> https://tzcentenary2017.wordpress.com/2018/01/06/fomu-ya-uongozi-chama-cha-skauti-tanzania/ thttps://www.scout.org/tanzania pia waweza kupata fomu ya uongozi kwa barua pepe ya: szone2012@live.com au dsmscout@gmail.com
Waweza pia kupakua fomu hii kwa https://web.facebook.com/SCF360