Powered by: Elbahsan Web & Blog Designer
Do want your Network!!! Website or Blog-Spot, Try Us: Elbahsan Web & Blog Designer Contact Us Now... Calll; +255743550360 | +255788680558 Email; murtadhaalbahsan@gmail.com

Zawamba Photo Production

Jumatatu, 26 Novemba 2018

Wakosa Dhamana kwa Mara ya Tatu: Amber Rutty na Mpenzi wake Warudishwa tena Segerea

 
Msanii Rutyfiya Abubakary maarufu kama ‘Amber Ruth’ na mpenzi wake Said Bakary Kitomali wamekosa tena dhamana kwa mara ya tatu katika kesi inayowakabili ya kufanya mapenzi kinyume na maumbile.

Mbali na Amber Ruth na Said Bakary, mshtakiwa mwingine ni James Charles maarufu kama ‘James Delicious’ ambaye yeye yupo nje kwa dhamana.

Mshtakiwa Amber Rutty alimueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Augustine, Rwezire kuwa mdhamini wake mmoja amefika mahakamani hapo lakini mwingine bado hajafika.

Baada ya kueleza hayo, Hakimu Rwezire amemwambia Amber Rutty kwamba dhamana ipo wazi na shughuli za mahakama zinaisha saa 9 alasiri hivyo wadhamini wake wakikamilika atadhaminiwa.Kesi imeahirisha hadi December 10,2018.

Katika kesi hiyo kosa la kufanya mapenzi kinyume na maumbile linamkabili Amber Ruth, ambapo anadaiwa amelitenda kati ama baada ya October 25, 2018 ambapo alimruhusu Said Bakary kumuingilia kinyume na maumbile, kosa ambalo amelikana.

Pia kosa jingine la kufanya mapenzi kinyume na maumbile, linamkabili mshtakiwa wa pili Said Bakary ambapo anadaiwa kati ama baada ya October 25,2018 jijini Dar es Salaam alifanya mapenzi na Amber Rutty kinyume na maumbile ambapo alisema si kweli.

Kosa la tatu la kuchapisha video ama picha za ngono, ambapo linamkabili James Charles ama James Delicious akidaiwa kati ya October 25,2018 alisambaza video za ngono kupitia magroup ya Whatsapp.

Kosa jingine la nne ni kusababisha kusambaa picha za ngono linamkabili Amber Ruth na Said Aboubakary ambapo wanadaiwa kati October 25,2018 walisababisha kusambaza picha za ngono kupitia makundi ya Whatsapp. Kosa ambalo wamesema si kweli.

Ili Amber Rutty na mpenzi wakewadhaminiwe wanatakiwa kutimiza masharti ya kuwa na wadhamini 2 ambapo kila mtu atasaini bondi ya Shilingi Milioni 1

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni