Powered by: Elbahsan Web & Blog Designer
Do want your Network!!! Website or Blog-Spot, Try Us: Elbahsan Web & Blog Designer Contact Us Now... Calll; +255743550360 | +255788680558 Email; murtadhaalbahsan@gmail.com

Zawamba Photo Production

Jumamosi, 6 Mei 2017

Rwanda: Picha za utupu za Diane Rwigara anayetaka kuwa Rais Rwanda zavuja

Picha za utupu za Diane Shima Rwigara zimezagaa katika makundi ya Whatsapp mjini Kigali, Rwanda.

Rwigara, 35, ni msichana ambaye juzi alitangaza nia yake ya kugombea urais katika uchaguzi utakaofanyika Agosti, 2017.

Picha zake za utupu zimetumwa kama barua-pepe kwa vyombo vya habari na mtu aliyejiita Twahirwa Emmy.

Bw Twahirwa amejitambulisha kuwa ni mwandishi wa habari aliyechukizwa na maadili ya mgombea huyo mtarajiwa.

Ingawaje hakuna chombo cha habari kilichorusha picha hizo kufikia sasa, lakini zimekuwa ‘habari ya mjini’ baada ya kutapakaa katika mitandao ya kijamii hususan Whatsapp.

Picha moja inamuonesha msichana huyo akiwa amekaa kwenye sofa nyumbani sehemu isiyojulikana, akiwa hajavaa chupi wala sidiria.

Picha nyingine inamuonesha akiwa amesimama huku ameyashika maziwa yake.

Ni picha ambazo zitakuwa zimepigwa na mtu wake wa karibu kwani inavyoonekana hazijapigwa kipaparazi.

Msichana huyo anaonekana pichani akiwa anamuangalia mpiga picha.Picha ya tatu inawaonesha watu wanne wakiwemo waandishi wa habari watatu wanaojulikana nchini Rwanda.

Mtuma picha ameahidi kutuma nyingine akidai lengo lake ni kuufahamisha umma kuwa mtu anayepiga picha za utupu hafai kupewa dhamana ya kuongoza nchi.

Rwigara ni msichana wa mfanyabiashara mashuhuri Asinapol Rwigara aliyefariki katika ajali ya barabarani mnamo Februari 2015.

Juzi, Jumatano, alitangaza nia yake ya kuwania urais, akiwaahidi Wanyarwanda kupambana na umaskini huku akiupa kipaumbele uhuru wa maoni endapo watamchagua.
Credit: Habari Pevu

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni