Powered by: Elbahsan Web & Blog Designer
Do want your Network!!! Website or Blog-Spot, Try Us: Elbahsan Web & Blog Designer Contact Us Now... Calll; +255743550360 | +255788680558 Email; murtadhaalbahsan@gmail.com

Zawamba Photo Production

Jumatatu, 26 Novemba 2018

Sheria mpya ya Mafao: SSRA watoa ufanunuzi

 
Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii SSRA, kupitia Mkurugenzi Mkuu, Irene Isaka, imekanusha malalamiko ya kupunguzwa kwa mafao ya wastaafu kupitia kanuni mpya za mwaka 2018 na kudai kuwa, taratibu zinazotumika ni za mwaka 2014.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam, Irene Isaka amesema changamoto hiyo inasambazwa na wanachama wachache, pia ni jambo ambalo linaweza kuzungumzika na kuongeza kuwa sheria ambayo imepitishwa inalenga kuifanya mifuko hiyo pamoja ili ilete faida kwa wanachama wake.

“Sheria ya kuunganisha mifuko imeleta usawa wa wanachama, kwa viwango wanavyochangia, kupunguza gharama za uendeshaji, jambo lingine ni kuweka uwaniano kati ya wachangiaji na wastaafu, lakini sasa tuna uwiano mzuri, pia sasa hivi hata akifariki mafao yataendelea kwa miaka 3,” amesema Kisaka.

Isaka ameeleza kuwa, haikuwa sahihi kundi dogo kulipwa mkupuo mkubwa wa zaidi ya mara tatu ya michango aliyochanga kwa kipindi chote cha ajira yake tofauti na wenzao hivyo, asilimia 25% iliyopunguzwa kwenye mkupuo imewekwa kwenye pensheni ya kila mwezi ambayo imeongezeka kwa asilimia 50%.

“Sheria hii imetatua changamoto, kwa hiyo niwaondoe wasiwasi lengo ni zuri na hata wanaolalamika ni wachache kwa sababu tunawastaafu zaidi ya laki moja kwa hiyo ni sehemu ndogo ya wanachama wenye hofu,” ameongeza.

“Kuhusu wategemezi wameshalipwa wengi, kwa sheria mpya imeongeza mafao na maslahi kwa wanachama wetu, ndiyo maana watu wengine kutoka nchi za Burundi, Namibia wamekuja kujifunza kwetu kwa sababu tumefuata vizuri kanuni za shirika la kazi duniani 'ILO'.”

Novemba 22 mwaka huu, Mbunge wa Bunda, Ester Bulaya alisema “tuliwaambia dhamira ya kuunganisha mifuko ya hifadhi ya jamii ilikuwa ni serikali kukwepa madeni inayodaiwa na mifuko ya hifadhi ya jamii ambayo kwa sasa inafikia trilioni 8 kwa sababu waliwekeza kwenye miradi isiyokua na tija,”

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni