Powered by: Elbahsan Web & Blog Designer
Do want your Network!!! Website or Blog-Spot, Try Us: Elbahsan Web & Blog Designer Contact Us Now... Calll; +255743550360 | +255788680558 Email; murtadhaalbahsan@gmail.com

Zawamba Photo Production

Jumatatu, 26 Novemba 2018

Polisi Anayetuhumiwa Kubaka Mtoto wa Miaka 13 Akosa Dhamana

Ofisa wa Jeshi la polisi mstaafu Mashaka Mdachi (72) amefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Morogoro kujibu shitaka la kumbaka na mwanafunzi wa darasa la tano mwenye miaka 13.

Mbele ya hakimu wa mahakama hiyo Elizabert Nyembele, mwanasheria wa Serikali Mary Lundu alidai mshtakiwa alitenda kosa hilo kati ya Januari 2017 na Oktoba 2018 katika nyakati tofauti huko Area Five kata ya kichangani Manispaa ya Morogoro.

Mwanasheria huyo alidai mahakamani hapo Ijumaa ya Novemba 23, 2018 kuwa mshtakiwa alifanya kitendo hicho huku akijua ni kosa kisheria na kumuathiri kisaikolojia binti huyo.

Alipotakiwa kujibu shitaka hilo mshtakiwa huyo alikana na mahakama Iliahirisha kesi hadi Desemba 6, 2018 itakapotajwa tena wakati polisi wakiendelea na upelelezi wa kesi hiyo na mshtakiwa alipelekwa rumande baada ya kukosa wa kumdhamini.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni