![]() |
| Dk. ali Mohamed shein, Raisi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar |
Na. Murtadhwa Elbahsan, Zanzibar
Rais wa Zanzibar Dk. Ally Mohamed Shein amemteua Ali Saidi Bakari kuwa Naibu Mkurugenzi Mku wa Mamlaka ya kudhibiti utafutaji na uchimbaji wa mafuta na Gesi asilia Zanzibar.
Kabla ya uteuzi huo Ali Bakari alikua Ofisa mwandamzi katika idara ya Nishati Zanziba.
Dk Shein amefanya uteuzi huo kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu Namba 53 cha katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, ambapo uteuzi huo unaanza leo.
Taarifa ya uteuzi huo imetolewa na kusainiwa na katibu wa baraza la Mapinduzi na katibu mkuu kiongozi Gk. Abdulhamid Yahya Mzee, leo tarehe 20 April 2017

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni