Mwanamuziki
ambaye amekuja kwa kasi kwenye tasnia ya, Harmorappa au muite Kiboko ya
Mabishoo hivi karibuni amewaacha midomo wazi watu wengi kufuatia jibu
lake alilolitoa alipoulizwa kuwa yeye ni mwanaume wa aina gani.
Akiwa katika kipindi cha Kikaangoni kinachorushwa na EATV,
Harmorappa aliulizwa swali lililotumwa na shabiki aliyekuwa akifuatilia
kipindi hicho ambalo liliuliza, “Wewe ni mwanaume wa aina gani?” na
akijibu swali hilo alisema, “Mimi ni strong woman.”
Jibu hilo limewashangaza wengi kwa sababu Harmorappa ni
mwanaume na hivyo wengi wameshindwa kuelewa kama alielewa swali
liliuliza nini au alijibu kama utani.
Alipoulizwa kama anafahamu lugha ya Kiingereza, Harmorappa alisema anaielewa vizuri lakini tatizo ni kwenye kuongea.
“LUGHA YA KIINGEREZA NAIFAHAMU VIZURI LAKINI ILE KUONGEA ONGEA NDIYO SIWEZI”
Aidha, amesema kuwa kwa sasa hana mpango wa kujiendeleza
kimasomo hasa kwenda chuo labda ajifunze zaidi lugha ya Kiingereza.
Kuhusu suala la kujiunga WCB, alisema, “Siwezi kujiunga WCB hata kwa
shilingi ngapi, Sizuzuki na hela, maana kama ni hela hata mimi mwenyewe
ninazo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni