Powered by: Elbahsan Web & Blog Designer
Do want your Network!!! Website or Blog-Spot, Try Us: Elbahsan Web & Blog Designer Contact Us Now... Calll; +255743550360 | +255788680558 Email; murtadhaalbahsan@gmail.com

Zawamba Photo Production

Jumatatu, 29 Mei 2017

Korea Kaskazini Yarusha Kombora Kuelekea Japan

Korea Kaskazini imerusha kombora la masafa mafupi, ambalo ni la tatu kurushwa na taifa hilo katika kipindi cha wiki tatu.

Kombora hilo aina ya Scud lilipaa umbali wa kilomita 450 (maili 280) kabla ya kuanguka katika maeneo ya bahari ya Japan, hatua iliyoifanya Japan kulalamika vikali.

Wachambuzi wanasema jaribio hilo ni ishara kwamba Korea Kaskazini inapiga hatua katika kuunda makombora yanayoweza kubeba mabomu.

Korea Kaskazini imeendelea kukiuka azimio la Umoja wa Mataifa linaloizuia kufanya majaribio yoyote ya makombora au silaha za nyuklia, na imeongeza kasi na idadi ya majaribio hayo katika miezi ya karibuni.

Kikosi cha Jeshi la Marekani katika Bahari ya Pasifiki kimesema kombora hilo lilirushwa kutoka Wonsan, Korea Kaskazini na lilipaa kwa karibu dakika sita kabla ya kuanguka.

Waziri Mkuu wa Japan Yoshihide Suga amewaambia wanahabari kwamba kombora hilo lilianguka katika eneo la bahari lililo kati ya visiwa vya Sado na Oki nchini Japan, katika eneo la pamoja la kiuchumi la visiwa hivyo viwili.

Msemaji wa Jeshi la Korea Kusini amesema kombora hilo lilipaa juu hadi kilomita 120 angani, na tathmini inaendelea kubaini “idadi hasa ya makombora yaliyorushwa,” ishara kwamba huenda nchi hiyo ilirusha zaidi ya kombora moja.

Jaribio hilo la kombora limetekelezwa siku moja baada ya vyombo vya habari vya serikali nchini Korea Kaskazini kusema nchi hiyo ilifanyia majaribio mfumo mpya wa kudungua ndege za kivita, na kutoa picha za kiongozi wa nchi hiyo Kim Jong-un alishuhudia majaribio hayo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni