
Majeruhi 
 wa ajali  ya gari iliyohusisha vifo 35 vya wanafunzi, walimu pamoja na 
dereva wa shule ya msingi Luck Vicent  wilayani Karatu, wamesafirishwa 
jana kwenda Marekani kwa ajili  ya matibabu zaidi .
Akizungumza katika uwanja wa ndege wa Kia, Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo alisema kuwa majeruhi hao wanasafirishwa na ndege ya Shirika la Samaritan Purse ili kuwawezesha kupatiwa huduma za matibabu zaidi ambazo zitaweza kurejeshea afya zao.
Gambo
 alisema kuwa Serikali imejitahidi kwa hali  na mali kuhakikisha kuwa 
wamewafariji wale wote waliofikwa na msiba na hata kuhakikisha kuwa 
majeruhi waliobaki wanapatiwa huduma ambazo zitaweza kunusuru maisha  
yao.
Gambo
 aliwataka wakazi wa jiji la Arusha na viunga vyake kuacha kutumia 
mitandao ya kijamii vibaya kwa kuwa inakwamisha huduma za kijamii kwa 
ajili ya kuchanganya na shuguli za kisiasa.
"Naombeni
 sana wana Arusha muache kutumia mitandao ya kijamii vibaya kwani hii 
mitandao imepotosha sana mambo mengi imehusisha huduma za kijamii kuwa 
mambo ya kisiasa hali ambayo inasababisha hata wanaojitokeza kuchangia 
maafa haya kuvunjika moyo kwa ajili ya mambo yaliyoandikwa kwenye 
mitandao ya hiyo"-alisema Gambo
Alidai
 kuwa huduma za kijamii hazipaswi kuhusishwa na shughuli za kisiasa 
kwani endapo zitahusishwa zitakwamisha hata wale wanaoendelea kufariji 
kushindwa kuendelea na moyo huo.
Mbunge
 wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu ambaye ni mmoja wa waliojitolea 
kufanikisha safari hiyo aliwataka Watanzania kuendelea kuombea majeruhi 
hao ili wapone haraka.
Safari
 ya majeruhi hao kuelekea Marekani ilianza saa 5:40 asubuhi wakiambatana
 na mkuu wa wilaya ya Hai, Gelasius Gaspa ambaye amemwakilisha mkuu wa 
mkoa wa Kilimanjaro, Meck Sadiki.




 
 
 
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni