Powered by: Elbahsan Web & Blog Designer
Do want your Network!!! Website or Blog-Spot, Try Us: Elbahsan Web & Blog Designer Contact Us Now... Calll; +255743550360 | +255788680558 Email; murtadhaalbahsan@gmail.com

Zawamba Photo Production

Ijumaa, 5 Mei 2017

Shilole afunguka na Sifa za Mwanaume Amtakae


Zuwena Mohamed ' Shilole' anayetamba na hit ya 'hatutoi kiki' amefunguka na kudai kwamba haitaji kuolewa na mwanaume mwenye pesa kwani wengi wao hutumia mali zao kama fimbo ya kuwachapa na  kunyanyasia wanawake zao.

Akiwa Kikaangoni kwenye ukurasa wa Facebook wa EATV, Shilole amefunguka kuwa yupo tayari kuolewa lakini mpaka atakapo pata mwanaume atakayekidhi vigezo vyake huku akitaja pesa siyo kitu anachokitanguliza bali heshima, upole na ukarimu.

"Natamani sana kuolewa lakini mpaka nimpate mtu mwenye vigezo ninavyohitaji mimi, napenda mwanaume anayejali, atakayeniheshimu lakini awe pia anafanya kazi kama hafanyi kazi simtaki. Lakini pia wanaume wenye pesa siwataki maana tunawaona huko majumbani wanavyotumia kama fimbo kuwanyanyasa wake zao" Shilole alifunguka.

"Mimi siangalii sana muonekano kwani unaweza kutengenezwa lakini ukiwa mfupi mimi sitakukubali nahitaji mwanaume mrefu na mwenye heshima na anayejituma kwenye utafutaji" aliongeza Shilole.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni