
BEKI wa Simba aliyesimamishwa na kamati ya masaa 72 kucheza ligi kuu kwa kosa la kumpiga ngumi kiungo wa Kagera Sugar George Kavilla Katika mchezo uliofanyika Kaitaba Bukoba na Simba kufungwa Kwa mabao mawili Kwa moja, Sasa yuko huru kuitumikia klabu yake ya Simba baada ya adhabu yake kuwa imeisha.
Kamati ya nidhamu ya shirikisho la Soka Tanzania (Tff) ilimpa Banda adhabu ya kukosa mechi mbili za ligi kuu kwa kosa la kumpiga ngumi Kavilla.
Kwa maana hiyo Banda yuko huru kuendelea kuitumikia klabu yake Kwani adhabu ya mechi mbili za mwanza Tayari alishazikosa simba ilicheza na Mbao Fc na kushinda Kwa mabao matatu Kwa mbili (3-2) baadae wakacheza dhidi ya toto African na kutoa suluhu (0-0) Michezo yote hiyo Simba wamecheza bila beki Wao Abdi Banda.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni