Powered by: Elbahsan Web & Blog Designer
Do want your Network!!! Website or Blog-Spot, Try Us: Elbahsan Web & Blog Designer Contact Us Now... Calll; +255743550360 | +255788680558 Email; murtadhaalbahsan@gmail.com

Zawamba Photo Production

Alhamisi, 20 Aprili 2017

Machozi ya Neymar dhidi ya Juventus yana mengi.


Baada ya klabu yake kushuhudia ikilazimishwa suluhu ya 0 kwa 0 na hivyo kuondolewa katika michuano ya UEFA ya msimu huu, mchezaji nyota wa timu hiyo Neymar Dos Santos aliangua kilio.

Neymar ambaye msimu huu anaonekana yupo katika kiwango cha hali ya juu alionekana akilia sana baada ya filimbi ya mwisho ya muamuzi wa mchezo huo, hali ambayo ilimfanya mchezaji mwenzake wa Brazil Dani Alves kujaribu kumbembeleza.

Inaonekana Barcelona walitaraji kufanya kile walichofanya katika mchezo wao dhidi ya PSG kwa kupindua matokeo ya bao 3 kwa 0 walizofungwa na Juve katika mchezo wao wa kwanza.

Baada ya matokeo kuja tofauti na walivyotarajia,ndipo mchezaji huyo alipatwa na masikitiko makubwa na kuanza kuangua kilio hicho kilichowasikitisha mashabiki wake na wa klabu hiyo kiujumla.

Lakini wengine wanaamini kiwango cha Neymar msimu huu kingekuwa na thamani kubwa zaidi kama angeiwezesha klabu yake ya Barcelona kuchukua kombe la Champions League.

Endapo Neymar angebeba Champions League msimu huu ingemuweka pazuri kushindania tuzo ya mchezaji bora wa dunia wa mwaka huu ambapo tayari watu wengi walishaanza kutaja jina lake katika tuzo hizo safari hii.

Lakini kutolewa kwao katika Champions League huku wakiwa hawana uhakika kuchukua kombe la La Liga msimu huu inaweza kutibua ndoto zake za kuwa mchezaji bora wa dunia,na hiyo ni kati ya sababu za machozi ya Neymar.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni