Powered by: Elbahsan Web & Blog Designer
Do want your Network!!! Website or Blog-Spot, Try Us: Elbahsan Web & Blog Designer Contact Us Now... Calll; +255743550360 | +255788680558 Email; murtadhaalbahsan@gmail.com

Zawamba Photo Production

Alhamisi, 13 Aprili 2017

Breaking News: Kibiti, Pwani: Majambazi yaua Askari Polisi SABA - Wapora Bunduki 7





Na Murtadhwa Elbahsan, Dar es salaam.
 
Habari zilizotufikia hivi punde, zimeeleza kuwa, askari polisi SABA wameuawa na majambazi huko Kibiti, Mkoani Pwani.

Habari hizo zinasema kuwa, askari hao wameuawa kwa kupigwa risasi na majambazi hao wakati wakijiandaa kuondoka kwenye lindo ambalo lilikuwa ni kizuizi cha barabarani ili warudi kituoni.

Imeelezwa kwamba majambazi hao waliwavamia ghafla polisi hao waliokuwa kwenye gari na kuwapiga risasi na kuwaua wote pale pale eneo la tukio, kisha kutokomea kusikojulikana.

  Inasemekana Majambazi hao walikua wanatumia silaha aina ya  SMG na Shambulizi limefanywa na mtu mmoja (jambazi)

Mmoja wa mashuhuda kutoka eneo la tukio ameeleza kama ifuatavyo;
"habari za usiku. Sisi huku BUNGU eneo la JARIBU mpakani tumepotelewa na askari saba(07) wa kikosi cha FFU.

Ilikuwa hivi:
Askari walikuwa wana-liviana ambapo section moja ilikuwa inatoka na nyingine inaingia. Sasa wakati hii inayotoka baada km 03, Jambazi/Gaidi lilikuwa limejificha porini karibu HIGHWAY baada ya gari kulikaribia jambazi/gaidi hili lilimshambulia dereva kwa mbele na gari kupoteza mwelekeo na kuanguka wakati huo jamba/gaidi liliendelea kushambulia."



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni