Powered by: Elbahsan Web & Blog Designer
Do want your Network!!! Website or Blog-Spot, Try Us: Elbahsan Web & Blog Designer Contact Us Now... Calll; +255743550360 | +255788680558 Email; murtadhaalbahsan@gmail.com

Zawamba Photo Production

Alhamisi, 13 Aprili 2017

Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamanda Mohamed Mpinga, DCP amekabidhiwa Cheti cha Pongezi

Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamanda Mohamed Mpinga, DCP akikabidhiwa Cheti cha Pongezi kilichotolewa na Asasi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania (AWAMATA) .


Na. Muhammad Shaban (Aluta.D), Dar es salaam
 
Leo tarehe 13 Aprili, 2017, Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamanda Mohamed Mpinga, DCP amekabidhiwa Cheti cha Pongezi kilichotolewa na Asasi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania (AWAMATA). Aliyekabidhi Cheti hicho cha Pongezi ni Ndg.Muhammad Shaban (Aluta.D) ambaye ni Mshauri Msaidizi wa Mwenyekiti-AWAMATA Taifa kwa niaba ya Chief Daudi Mrindoko ambaye ni Mwenyekiti-Taifa wa Asasi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania (AWAMATA). Awali kabla ya kumkabidhi Cheti hicho, alifikisha salamu na pole kwa Kamanda kwa msiba aliopata na pia kuomba dua kwaajili ya marehemu. Hafla hiyo fupi ilifanyika Makao Makuu ya Kikosi cha Usalama Barabarani. AWAMATA imetambua mchango mkubwa wa Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamanda Mohamed Mpinga, DCP katika kupungaza ajali nchini na kudhibiti madereva wazembe na pia uongozi mzuri wake mpaka kuanzishwa kwa ulipaji wa faini kwa njia ya kielektroniki na pia kuanzisha Speed Radars ambazo kwa kiasi kikubwa zimeanza kuleta heshima barabarani.
 


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni