Na. Murtadha Elbahsan.
Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji ametembelea
Tenki la Maji la terminal lilipo karibu na chuo kikuu cha ardhi ambalo
linapokea maji kutoka mtambo wa Ruvu na chini.
Pia ametembelea tenki kubwa jipya la Maji lilipo
Kibamba Luguruni ambalo linapokea maji kutoka mtambo wa Ruvu juu na
ametembelea Ofisi za Dawasco Mkoa wa Kibaha na kumalizia ziara yake kwa
kutembelea mtambo wa kuzalishia Maji wa Ruvu juu ambapo umeanza
kuzalisha maji mapya leo.
Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi wa DAWASA, mhandisi
Romanus Mwangingo, akitoa maelezo mafupi kwa Katibu mkuu Wizara ya Maji
na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo kuhusu tenki jipya la Maji lilipo
Kibamba Luguruni ambalo linapokea maji kutoka mtambo wa Ruvu juu mara
baada ya kufanya ziara ya kutembelea Mtambo huo wa uzalishaji Maji wa
Ruvu juu uliopo Mlandizi, mkoani Pwani. Picha na Emmanuel Massaka, Globu
ya jamii.
Ofisa Mtendaji mkuu Dawasco, mhandisi Cyprian
Luhemeja akitoa maelezo mafupi kwa Katibu mkuu Wizara ya Maji na
Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo katika ziara ya kutembelea Mtambo
Ruvu juu uliopo mkoani Pwani.
Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa
Kitila Mkumbo akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Wizara ya
Maji na Umwagiliaji
Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa
Kitila Mkumbo akizungumza na watumishi wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji
leo jijini Dar es Salaam.
Watumishi wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji wakimsilikiza Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo
Moja ya mitambo ya maji katika eneo la Ruvu Juu kama inavyoonekana.
Sehemu ya mtambo wa kusafirishia maji.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni